Ndege ya shirika moja la ndege la urusi,iliyokuwa na abiria zaidi ya mia mbili imeanguka katika eneo la Sinai nchini Misri. Ofisi ya waziri mkuu wa misri imethibitisha ajali hiyo na kusema ndege hiyo aina ya AIRBUS A-321 ilikuwa imetoka mji wa Sharm el-Sheikh ikielekea mji wa SAINTT PETERSBURG nchini Urusi ilipoanguka. Vyombo vya habari vya misri vimesema mabaki ya ndege hiyo yamepatikana na gari ishirini za kubebea wagonjwa zimetumwa eneo la ajali. Awali, kulikuwepo na utata kuhusu hatima ya ndege hiyo, kwa baadhi ya taarifa zilisema ajali hiyo ilitokea karibu na visiwa vya CYPRUS, lakini taarifa ya afisa katika ofisi ya waziri mkuu wa misri SHARIF ISMAIL imethibitisha kuwa ndege hiyo ilianguka katikati mwa eneo la Sinai na kuongeza kuwa ofisi hiyo imeunda kamati ya dharura ya kushughulikia ajali hiyo.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat