Watanzania wameonywa kuwa makini kwa kutokubali kuvurugwa na watu wanaotangaza nia ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, badala yake wafanye maamuzi sahihi kwa kumchagua kiongozi atakayekuwa tayari kulinda rasilimali za nchi na asiye mpenda rushwa. Kauli hiyo imetolewa na Benard Membe wakati akitafuta wadhamini mkoani Ruvuma ambapo wanachama zaidi ya elfu tano walijitokeza kumdhamini. Aidha aliwaomba wananchi wachague mtu ambaye atakuwa na uzalendo wa nchi na ambaye atalinda rasilimali za nchi na kusimamiapia asiwe penda rushwa. Mgombea huyo amesema ,iwapo wataridhika kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wa kuongeza watanzania zaidi ya milioni 45 hawana budi kumchangua. Katika hatua nyingine mgombea nafasi ya uraisi makongoro Nyerere pia aliwataka watanzania kuwa makini na wagombea na wawasikilize na badaye wachague mtu ambaye ataweza kulinda chama na masirahi ya watanzania FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat