Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all 2247 articles
Browse latest View live

Mgombea ‘wa nne’ aivuruga Ukawa

$
0
0

Dar es Salaam.  Wakati wa hali ya sintofahamu ikiwa imetawala uteuzi wa mgombea atakayeungwa mkono na vyama vinne vya upinzani, imebainika kuwa mzozo unaochelewesha suala hilo ni mgombea ambaye Chadema haijamuweka bayana. Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ndiye ambaye anapewa nafasi kubwa ya kupitishwa kugombea urais kwa tiketi ya Ukawa mbele ya mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na kada wa NCCR-Mageuzi, Dk George Kahangwa, lakini hadi sasa vyama hivyo bado vinasita kumtangaza mteule wake. Profesa Lipumba alikuwa amewaahidi waandishi wa habari wiki iliyopita kuwa mgombea ambaye ataungwa mkono na vyama hivyo vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD angetangazwa Julai 14, lakini siku hiyo hakuna aliyetangazwa. Badala yake viongozi wa Chadema, NLD na NCCR ndio waliofika Hoteli ya Coloseum jijini Dar es Salaam ambako Profesa Lipumba aliahidi kuwa ndiko jina la mgombea huyo lingetajwa, wakati viongozi wa CUF hawakuonekana na baadaye jioni wakasema kuwa walikuwa na kikao cha ndani ya chama cha kutafuta ufumbuzi wa mambo ambayo walikuwa hawajakubaliana. Vyama hivyo vitatu vikaeleza baadaye kuwa jina hilo litatangazwa ndani ya siku saba kuanzia Julai 14, lakini siku iliyofuata CUF ilisema suala la kuachia chama kingine jukumu la kusimamisha mgombea urais litawasilishwa kwenye kikao cha Baraza Kuu la chama hicho ambacho kitafanyika Julai 25, jambo ambalo lilikubaliwa na vyama hivyo vitatu. Matamko hayo yamefanya suala la mgombea urais wa Ukawa kugubikwa na giza nene, lakini kwa siku tatu Mwananchi imefuatilia na kubaini kuwa mgombea ambaye yuko na hajatajwa rasmi kwa vyama hivyo vinne ndiye anayechelewesha mchakato huo na amesababisha kuwapo na hatari ya umoja huo kuparaganyika. Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya vikao vya Ukawa vilivyoanza kufanyika takribani wiki mbili jijini Dar es Salaam, zinaeleza kuwa licha ya viongozi wa vyama hivyo kumpata mgombea wao wa urais katika kikao cha Julai 14 mwaka huu, walikwama kumtangaza kutokana na CUF kutokuwapo kikaoni ikielezwa kuwa wanapinga maendeleo ya mchakato huo. Taarifa hizo zinaeleza kuwa msimamo huo wa CUF umetokana na utata ulioibuka katika kikao cha Ukawa cha Julai 11 na 14, baada ya wagombea wawili kati ya watatu, kukubali mmoja wao agombee urais, lakini chama chake kikasema kuwa kinachotakiwa ni Ukawa kutangaza jina la chama kitakachotoa mgombea na si jina la mgombea. Tayari Profesa Lipumba ameshachukua fomu za kuwania urais kwa tiketi ya CUF, wakati Dk Kahangwa amechukua fomu kuwania urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, huku mchakato wa Chadema ukiwa haujaanza. Habari hizo zinaeleza kuwa awali kulikuwa na mvutano mkali kati ya Profesa Lipumba na Dk Slaa na kwamba katika kikao cha Julai 11, Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa CUF alikubali kumuachia Dk Slaa agombee urais kupitia Ukawa, lakini inaonekana hata ndani ya Chadema bado hawajaafikiana kuhusu jina la mgombea. Hata hivyo, chama hicho kimeeleza kuwa jina la mgombea urais limeshapatikana na linasubiri muda muafaka. “Tutamtangaza mgombea urais wa Ukawa ndani ya wiki moja kama tulivyosema awali,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, John Mnyika jana. “Wananchi wanatakiwa kutulia tu, siku ikifika tutatangaza.” Mnyika alitoa ufafanuzi huo muda mfupi baada ya kulieleza gazeti hili jana kwamba wanaopaswa kuzungumzia suala hilo ni Dk Slaa na Profesa Lipumba. Jibu kama hilo la Mnyika lilitolewa pia na mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alipoulizwa kuhusu habari kwamba kuna jina la mgombea urais linalosumbua Ukawa. “Sijui chochote kuhusu hilo. Ila watu hawa wawili, Mbowe na Dk Slaa watakusaidia kujua kuhusu jambo hilo.” Alipobanwa zaidi, alisema: “Unajua hata mimi nazisikia sana habari kama hizo pamoja na nyingine nyingi. Katika Ukawa watu wanazungumza ndani ya vikao na nje ya vikao, ila wa kulithibitisha hilo ni hao watu wawili niliokutajia.” Lakini mpashaji habari wetu alisema ugumu wa kumpata mgombea urais wa Ukawa kutoka Chadema unasababishwa na chama hicho kutotaka kuweka bayana jina la mtu atakayebeba jukumu hilo wakati wameshakubaliana kuwa Dk Slaa ndiye asimamishwe. “Inaonekana kama kuna mtu mwingine hivi. Wote tumekubali mgombea awe Dk Slaa, lakini Chadema wenyewe wanazuia asitangazwe,” alisema mpashaji huyo kutoka ndani ya vikao vya Ukawa. Habari zaidi zinaeleza kuwa ndani ya Chadema kuna mvutano, kwani wapo wanaotaka Dk Slaa atangazwe kuwa ndiye mgombea na wanaotaka asitangazwe lakini hawaweki bayana kuwa hawamtaki au wanataka mtu mwingine. Hata hivyo, habari hizo zinasema kuwa sababu nyingine inayochelewesha suala hilo ni Chadema kutotaka kumtangaza mgombea wake kutokana na mchakato wake wa uteuzi wa mgombea urais kutoanza. Mchakato huo utaanza Julai 20 na kumalizika Julai 25, siku ambayo CUF itakuwa na kikao chake cha Baraza Kuu kuamua mgombea urais. Habari zinasema kuwa Chadema imekuwa ikisisitiza kuwa Ukawa itaje jina la chama kitakachotoa mgombea urais na si jina la mwanachama atakayegombea nafasi hiyo. Habari hizo zinaeleza kuwa chama hicho kinachoongoza kambi ya upinzani, kinadai kuwa Ukawa kutangaza jina la mwanachama atakayegombea urais ni kuingilia mchakato wa Chadema ambao humalizika kwa kikao cha juu kupitisha mgombea urais wa chama. Awali baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya CUF, Profesa Lipumba alikuwa akisema kwenye mikutano ya hadhara kuwa vyama hivyo vinne vimekubaliana kuwa kila kimoja kifanye mchakato wake wa kupata mgombea. Alisema kila chama kitalazimika kupeleka Tume ya Uchaguzi (NEC) jina la mgombea wake ili kiwe na uhakika kuwa amepitishwa halafu ndipo vikutane na kuamua mmoja atakayeungwa mkono na vyama vyote. Lakini hali hiyo ilibadilika mwishoni mwa mchakato wa CCM wa kumpata mteule wake wa mbio za urais baada ya Ukawa kuitisha mkutano wa pamoja na wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo ambao habari zinasema walishinikiza kuwa mgombea wa Ukawa atangazwe mapema na si kusubiri mchakato wa kila chama. Mvutano ndani ya Ukawa ulianza wakati CUF ilipotaka iachiwe nafasi ya kusimamisha mgombea urais kwa madai kuwa Chadema imeshaunda mtandao mzuri na hivyo itakuwa na nafasi ya kuingiza wabunge wengi, lakini chama hicho kinachoongoza kambi ya upinzani bungeni kikaeleza kuwa CUF ilishaachiwa nafasi ya kusimamisha mgombea urais wa Zanzibar. matukio hayo yanatokea wakati aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa akiombwa asiondoke CCM baada ya kuenguliwa kwenye mchakato wa urais wa chama hicho tawala. Makada kadhaa wamejitokeza hadharani na kumsihi mbunge huyo wa Monduli kukubali matokeo na kutofanya uamuzi wa kuondoka, huku watu wanaosema kuwa wanachama wa CCM wakitangaza kujivua uanachama na kujiunga na Chadema kwa maelezo kuwa hawakubaliani na uamuzi wa chama hicho tawala kumuengua Lowassa. Lowassa hajatoa kauli baada ya kuenguliwa CCM na mapema wiki hii kulikuwa na habari kuwa angeongea na waandishi wa habari, lakini mkutano huo ukafutwa saa chache kabla ya kuanza.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Wazee wa kimila sasa wamwangukia Lowassa

$
0
0

Arusha. Wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimaasai (Malaigwanan) kutoka Wilaya ya Monduli wamemuomba waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kubaki na kuendelea kuwa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu ndicho kilichomlea na anakijua. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Monduli kwa niaba ya Malaigwanan, Mzee Joseph Mesopiro kutoka Kata ya Sepeko wilayani humo alisema viongozi wa mila wanakusudia kutuma ujumbe maalumu kwa Lowassa kumshauri asihame CCM kama baadhi ya watu aliowaita wapambe wanavyomshauri. “Sote Monduli tumesononeka kwa jinsi vikao vya chama vilivyomtendea mbunge wetu. Bado tunampenda kama ambavyo tunakipenda chama chetu. Tunaamini ataendelea kubaki CCM na kupigania ushindi wa chama katika uchaguzi ujao,” alisema Mzee Mesopiro Alizungumza hayo wakati wa hafla ya kuchukua fomu na kuomba kuteuliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Monduli, mwanasiasa wa siku nyingi Loata Sanare. Kwa upande wake Laigwanan Julius Laizer kutoka Kata ya Moita, alisema licha ya mizengwe iliyotawala vikao vya uteuzi vya CCM vilivyomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha ufa miongoni mwa viongozi na wanachama, bado anaamini chama hicho kitaendelea kubaki imara hata kama baadhi ya watu watakihama. “Kama viongozi tuliolelewa na kukuzwa na CCM, tunaamini chama hiki kitaendelea kuwa imara na hatuko tayari kukubali ushawishi wowote wa kututaka tuhamie upinzani,” alisema Laizer. Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Lepurko wilayani Monduli, Njoput Alami alibeza taarifa za kushawishi watu kuhama CCM kwa kisingizio Lowassa kukatwa akiziita ni kelele za wapambe wanaohofia kukosa fursa walizozitarajia iwapo Lowassa angeteuliwa kuwa mgombea wa CCM. Akizungumzia taarifa za wanaCCM wilayani Monduli kughadhabika na kutishia kukihama chama hicho kutokana na Lowassa kukatwa, Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro alikiri baadhi ya wanachama kuchana kadi na kuchoma bendera za chama hicho, lakini akasema ni idadi ndogo ikilinganishwa na wanachama waliopo wilayani humo. “Kuna taarifa za kadi na bendera za CCM kuchomwa moto katika baadhi ya maeneo kama Migungani, Mto wa Mbu, Makuyuni na Nalaarani. Tunaendelea kukusanya taarifa sahihi na kufanya tathmini ya matukio hayo,” alisema Kimaro.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Lembeli: Sitagombea ubunge kupitia CCM

$
0
0

Mbunge wa Kahama, James Lembeli ameiweka njiapanda CCM baada ya kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho. Uamuzi wa Lembeli umekuja wakati wanachama kutoka sehemu mbalimbali wakitangaza uamuzi wao wa kujiengua CCM na kujiunga na vyama vya upinzani, hasa Chadema ambayo imesomba asilimia kubwa ya wahamaji hao. Akizungumza jana baada ya kuzagaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa amekihama chama chake na kuhamia Chadema, Lembeli alisema taarifa hizo ni uvumi uliozagaa jimboni kwake, lakini hajajiunga na chama chochote. “Ni uvumi tu na uvumi wenyewe umechangiwa na swali nililoulizwa leo na wananchi kwamba ‘mbona toka mchakato wa kuchukua fomu umeanza hatujakuona’ na mimi nikawajibu kuwa ‘sitachukua fomu’,” alisema. Lembeli (pichani) alisema amechukua uamuzi huo kutokana na rafu inayoendelea jimboni humo na maneno ya baadhi ya wanachama, wakiwemo viongozi kuwa hatakiwi na vigogo ndani ya CCM. Lembeli, mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele wakati wa kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, alisema sababu za kutotakiwa huko zinatokana na dhana potofu ya baadhi ya viongozi kwamba michango yake ndani na nje ya Bunge inaivua nguo Serikali. “Tangu mchakato wa uchukuaji wa fomu umeanza baadhi ya wanachama wengi tu wameitwa kwenye vikao visivyo halali karibu kata zote wakiwa na kadi zao na kuorodheshwa na kupewa maagizo ya kunikataa kwenye kura ya maoni na wengine wanapewa Sh5,000,” alisema Lembeli alidai kuwa mbaya zaidi ni kwamba zipo kadi mpya za CCM zinazotolewa kiholela bila kufuata utaratibu na licha ya kulalamikia hali hiyo hakuna hatua zilizochukuliwa. Alisema kutokana na yote hayo, aliwahi kusema kwenye mkutano wa hadhara kuwa kuna njama hizo, lakini badala ya CCM kufanyia kazi madai hayo, wakamuita mbele ya Kamati ya Maadili. “Kwenye kamati ya maadili nilituhumiwa kuwa nakidhalilisha chama na kutakiwa niwataje nani walioniambia sitakiwi. Niliwajibu, tena kwa maandishi na kuwapa orodha, lakini mpaka leo kimya ina maana mimi bado ni mtuhumiwa,” alidai. “Mimi siyo mtoto mdogo. Naelewa nini kinaendelea na ndiyo maana nimesema sitachukua fomu ya kugombea ubunge kwa mazingira haya. Bado sijatangaza kuhama CCM”. Wakati Lembeli akisisitiza suala la kuhama kwake ni fununu tu, habari nyingine zilidai huenda akagombea ubunge kwa tiketi ya Chadema kutokana na kutokubaliana na mchakato huo anaodai ni batili. Lembeli anaonekana kuwa mwiba ndani ya Serikali ya CCM baada ya kuiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ya Bunge katika uchunguzi wa uendeshaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili na kuibuka na taarifa iliyoonyesha kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Mawaziri hao ni Balozi Hamis Kagasheki, Dk. David Mathayo, Dk. Emmanuel Nchimbi, Shamsi Vuai Nahodha na Ezekiel Maige. Lembeli pia nusura ajikute nje ya mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2010 wakati alipopigiwa simu na katibu mkuu wa CCM wa wakati huo, akiambiwa achukue fomu za kuwania ubunge wa jimbo jipya la Ushetu. Wakati huo, Lembeli alidokezwa siku ya mwisho na ofisa mmoja wa Tume ya Uchaguzi kuwa hakukuwapo na jimbo hilo na kulazimika kufanya jitihada katika muda mfupi kuchukua fomu kwenye Jimbo la Kahama na kufanikiwa kushinda kiti hicho. Hivi karibuni, Lembeli alitofautiana na taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ya kuwasafisha mawaziri na katibu wa wizara waliowajibika kutokana na kashfa ya escrow na Operesheni Tokomeza. Lembeli alisema kitendo cha kuwasafisha viongozi hao ni kuipeleka nchi gizani. “Yuko hapa (waziri mkuu wa zamani, Edward)Lowassa. Japo mimi sipendi wizi na ufisadi, katika kashfa ya Richmond nilikuwa mmoja wa waliopiga kelele awajibike. Lakini wengine wamesafishwa, kwanini naye asisafishwe,” alisema baada ya taarifa hiyo ya Ikulu. “Kama ni kusafishana tusafishwe wote, tuanze upya ndipo nchi hii itatawalika, vinginevyo huko mbele kuna giza nene.”

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mwinyi Avunja Ukimya Kilichotokea Dodoma…… Asema Haikuwa Kazi Rahisi Kumpata Mgombea wa Chama

$
0
0

Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa shughuli ya kupata mgombea urais kwa tiketi ya CCM haikuwa rahisi na akashukuru kwamba imemalizika kwa amani. Mchakato huo ulihitimishwa Julai 12 mjini Dodoma wakati Mkutano Mkuu wa CCM ulipopitisha jina la Dk John Magufuli kugombea nafasi ya kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake mwishoni mwa mwaka. Jumla ya makada 38 walijitokeza kuwania nafasi hiyo, na majina matano ndiyo yaliyopitishwa kwenda Halmashauri Kuu na baadaye matatu kwenda Mkutano Mkuu. Mchakato wa urais ndani ya CCM ambao kwa kawaida hutawaliwa na msuguano kabla ya kumalizika kwa maridhiano, safari hii ulienda mbali zaidi baada ya wajumbe watatu wa Kamati Kuu kupinga nje ya kikao uamuzi wa chombo hicho na baadaye wajumbe wa Halmashauri Kuu kumwimbia mwenyekiti wao, Jakaya Kikwete wimbo wa kuonyesha wana imani na Edward Lowassa baada ya jina la mbunge huyo wa Monduli kuenguliwa na Kamati Kuu. Jana, akitoa hotuba fupi baada ya kumalizika kwa sala ya Eid el Fitr kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mwinyi alizungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu mchakato huo, akidokeza hali ilivyokuwa. “Haikuwa kazi rahisi kwenye mchakato huu wa kumtafuta mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM,” alisema Mwinyi lakini akawahi kuipoza kauli hiyo kwa kuelezea amani ilivyotawala mwishoni. “Kama ni jahazi basi sasa tunashukuru limefika pwani salama.” “Uchaguzi huu ni kwa ajili ya kuwapata viongozi wetu, tunataka viongozi bora wa kutuletea maendeleo, mapatano na wenye mahaba na wananchi.” Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya mchakato huo wa kumtafuta mgombea wa urais kukamilika mjini Dodoma, Mzee Mwinyi alimshukuru Mungu kwa mchakato huo kuisha salama. “Haikuwa kazi rahisi kwenye mchakato huu wa kumtafuta mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM, kama ni jahazi basi sasa tunashukuru limefika pwani salama. “Sasa, ninawaomba Watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi wa nchi tunaoufanyika kila baada ya miaka mitano,“ alisema Rais Mwinyi ambaye alikuwa mmoja ya wajumbe wa Baraza la Ushauri waliofanya kazi ya kutuliza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hadi kuafikiana kuendelea na mchakato wa kumpata mgombea urais. Aliwasisitizia Watanzania kuacha tabia ya kupenda mno na kuacha kubaguana, akisema hakuna aliye bora na kuwataka kuzidisha mapenzi miongoni mwao na kusherehekea vyema Sikukuu ya Eid el Fitr. “Hakuna jambo lenye maana kama hili la kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye kutufikisha salama siku kama hii ya leo (jana) ambayo tunasherekea Sikukuu ya Eid,” alisema Mwinyi. Awali Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum aliwasisitizia wananchi umuhimu wa kusherekea sikukuu hiyo katika hali ya amani na utulivu. Pia, aliwashauri wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao sehemu zenye maadili ili washerehekee kama ambavyo Mwenyezi Mungu anapenda. “Leo (jana) ni siku ya furaha, naomba tusherekee maeneo salama pia Waislamu msisahau kufunga sita kwani ina malipo makubwa,” alisema Alhad Salum. Mkoani Geita ambako ilifanyika sala ya kitaifa ya Eid, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal alihutubia Baraza la Eid na kusema kipindi hiki kinahitaji utulivu, kuelewa na kuheshimiana pamoja na kudumisha uhusiano ili Taifa lipate viongozi bora. “Tuwe watulivu ili Tanzania ibaki kuwa nchi ya kukimbiliwa na isiwe nchi ya kukimbiwa… sisi tusiwe wakimbizi, tuwe watu wa kupendana, kuvumiliana na kuthaminiana. Tusifikie hatua ya kuchukiana, kuuana na kufanyiana ukatili,” alisema Dk Bilal. Alisema amani inaweza kuvunjwa na mtu yoyote kwa namna yoyote ile, akaharibu mazuri na heshima ya Taifa na akawaomba wananchi na waumini wote wasifikie hatua hiyo akisema ndiyo wenye uwezo wa kuifanya nchi yao kuwa ya amani. “Tuishi kwa kuheshimiana, kupendana na kuvumiliana tushikamane katika, hali iliyopo sasa kwa nchi yetu siyo nzuri. Si ajabu hivi sasa tunavyoongea kuna sehemu mabomu yametokea, si ajabu kuna watu wameuawa kikatili. Hii yote ni sababu watu sasa wanapoteza misingi ya kuheshimiana, upendo na kuvumiliana,” alisema Bilal kwenye Viwanja vya Karangara. Awali Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania, Bakwata, Sheikh Suleiman Lolela alisema waumini na wananchi wote waitumie vyema nafasi ya Uchaguzi Mkuu kuhakikisha wanachagua viongozi bora watakaoendeleza amani. Kisiwani Unguja, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amewataka viongozi wa vyama vya siasa, taasisi za kijamii na madhehebu ya dini kulinda na kuheshimu msingi na malengo ya kuanzishwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba. Akiuhutubia kwenye Baraza la Eid el Fitr lililofanyika Ukumbi wa Bwawani na kuhudhuriwa pia na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad jana, Dk Shein alisema viongozi wa kisiasa wanapaswa kufanya siasa kwa kuzingatia misingi ya Katiba na sheria kwa madhumuni ya kuendeleza na kulinda amani na umoja wa kitaifa kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake. “Tunaweza kushindana bila ya kulaumiana, kukejeliana na tunaweza kushindana bila ya kudharauliana au kuhasimiana,” alisema Dk Shein kwenye shughuli hiyo iliyotaliwa na hali ya utulivu. Alieleza kuwa vyama vya siasa vimeanzishwa na vipo kwa ajili ya kushindana kwa sera kwa madhumuni ya kuchochea maendeleo ya Zanzibar na siyo kugombanisha watu na kuvuruga misingi ya amani na umoja wa kitaifa. Kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, sheikh wa mkoa, Ahmed Zuber aliwataka Watanzania kudumisha amani na umoja. Zuber alisema dunia sasa imechafuka kutokana na uvunjifu wa amani unaochochewa na siasa chafu hivyo Watanzania bila kujali dini wala itikadi zao wanapaswa kuilinda amani iliyopo sasa. “Tunahitaji utulivu. Nchi nyingi huharibikiwa kipindi kama hiki cha uchaguzi, amani hupotea kipindi hiki cha uchaguzi. Ndugu zangu Waislamu na msio Waislamu tukiichezea amani hii iliyopo sasa, tujue hakika hatuna kwa kukimbilia,” alisema.Mkoani Tanga, imamu wa Msikiti wa Ibadhi, Sheikh Mohammed Said aliitaka jamii kudumisha amani na utulivu uliopo na kuacha kushabikia vyama vya siasa. Sheikh huyo alisema ni wajibu wa kila mtu kutambua kuwa amani iliyopo ikitoweka ni vigumu kuirejesha na hivyo kila mmoja ahakikishe anatambua wajibu wake. Alisema wakati wa uchaguzi, hutokea jamii kuhamasishana kwa mambo ya kisiasa, jambo ambalo alisema ni baya na halifai kutokea na hivyo kutaka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake.Mkoani Lindi, Sheikh Salimu Nalinga akitoa salamu za Eid el Fitr aliwataka Waislamu kuchagua viongozi waadilifu ili kuifanya nchi kuendelea kuwa ya amani na utulivu.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Hali ni Mbaya: Madiwa 20 wa CCM, Wenyeviti 6 Wa Vijiji na Viongozi wa Jumuiya za CCM Monduli kwa Lowassa Wahamia CHADEMA

$
0
0

WAKATI wakongwe wa siasa wakimhadharisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kutofuata mashabiki wanaomtaka ahame CCM ambako amelelewa na ndiko anakoheshimika, madiwani 20 wa chama hicho katika Jimbo la Monduli, wamejiunga na Chadema. Madiwani hao wameingia Chadema na kufuatwa na wenyeviti sita wa vijiji pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM, huku wakimwomba Lowassa ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo, kufanya kinachoitwa ni uamuzi mgumu wa kuwafuata, baada ya CCM kukata jina lake sambamba na wagombea urais wengine 33, wakiwemo waliowahi kuwa mawaziri wakuu kama yeye. Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara, kabla ya kukabidhi kadi yake na za wenzake 19 wa CCM kwa viongozi wa Chadema, kiongozi wa Madiwani hao, Julius Kalanga kutoka Kata ya Lepurko, alisema wamefanya uamuzi aliouita mgumu, ambao Lowassa amekuwa akiuzungumza. “Sisi tumeamua kujiunga Chadema kutafuta haki na kuondoka CCM ambako wanachakachua Katiba ya Chama kwa kumpitisha kiongozi wanayemtaka, badala ya kufuata Katiba na wananchi wanachotaka. “Tunamwomba Mheshimiwa wetu Lowassa, atufuate huku Chadema, afanye uamuzi mgumu aliokuwa akisema kila siku na asiogope kuhama… atakuwa amefanya uamuzi wenye tija kwa Taifa,” alisema Kalanga. Diwani huyo pia aliwasihi wananchi kufuata madiwani wao wanakokwenda kwa sababu hata huko watachukua fomu na kugombea ili kuing’oa CCM madarakani. Waliohama Madiwani waliohama chama ni wa kata ya Engaruka, Engutoto, Esilalei, Loksale, Majengo, Makuyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mferejini, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashaini. Madiwani na viongozi hao ni Kalanga mwenyewe, Edward Lenanu, Bazir Siamini, Sigur Olekibinti, Loti Yamat, Goodluck Lerunya, Pashet Sengurumi, Yase Runja, Gidion Kimongishu, Dora Kipuyo, Mary Morindat, Sara Lomayan na Halima Lusinde. Wengine ni Dotto Mlacha, Hawa Nyambiry, Alex Kamanda, Sion Kapela, Maria Lemta, Onesmo Naikoyo, Shaban Adam, Enditosidai Naikulo na Elifuraha Simon. Pia yupo Dinna Solomon, Loti Naparana, Jocy Laizer, Edward Mathayo, Piniel Loning’o, Napir Mukare, Inot Leringa, Kalaine Lowassa, Maria Mepukori, Mary Stivin na Edward Kone. Ushauri wa wakongwe Mwito huo wa madiwani wa Monduli, unatofautiana na ushauri wa kada mkongwe wa CCM, Steven Mashishanga, aliyekaririwa akimtaka Lowassa atulie na aachane na ushawishi wa watu wanaomtaka ahame chama hicho. Mashishanga katika mahojiano yake na gazeti moja la kila siku juzi, alimkumbusha Lowassa kuwa bado ni kiongozi anayeheshimiwa na jamii na kumuasa kuwa kama anahisi ameonewa, asamehe. Akifafanua hoja zake, Mashishanga alisema wanaomshawishi Lowassa ahame CCM na wale wanaohama chama hicho kwa sababu ya kukatwa kwa jina la Lowassa katika kuwania urais, si wana CCM wa uhakika. Kwa mujibu wa Mashishanga, ndani ya CCM mgombea akiteuliwa, wanachama huachana na yaliyopita na kuwa wamoja kwa ajili ya kukiendeleza chama. Malaigwanani Mbali na Mashishanga, pia wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimasai, maarufu malaigwanani kutoka Wilaya ya Monduli, nao wamemuomba Lowassa kuendelea kuwa kada wa CCM, kwa sababu ndicho chama kilichomlea na anakijua. Mmoja wa malaigwanani, Mzee Joseph Mesopiro, kutoka Kata ya Sepeko, alikaririwa na vyombo vya habari kwa niaba ya malaigwanani akisema, wanakusudia kutuma ujumbe maalumu kwa Lowassa, utakaomshauri asihame CCM kama baadhi ya watu aliowaita wapambe wanavyomshauri. Laigwanani mwingine, Julius Laizer kutoka Kata ya Moita, alisema bado anaamini kuwa CCM itaendelea kubaki imara, hata kama baadhi ya watu watakihama. Lazier alisema viongozi waliolelewa na kukuzwa CCM, wanaamini chama hicho kitaendelea kuwa imara na hawako tayari kukubali ushawishi wowote wa kutaka wahamie upinzani. Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lepurko wilayani Monduli, Njoput Alami, alikaririwa akibeza taarifa za kushawishi watu kuhama CCM kwa kisingizio cha Lowassa kukatwa katika majina ya wawania urais, akiziita ni kelele za wapambe wanaohofia kukosa fursa walizotarajia, iwapo Lowassa angeteuliwa kuwa mgombea urais wa CCM. Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa aliwakaribisha na kusema Chadema watu wote wanapendana na hakuna ukubwa wala uongozi, hivyo wanapokuja huko ni kazi moja ya ukamanda kuwatumikia wananchi.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Aliyechana Fomu Ya BVR kwa Kukataa Kuvua Hijab Atiwa Mbaroni

$
0
0

WATU wawili wamekamatwa katika vituo viwili tofauti vya uandikishwaji wa daftari la mpigakura kwa kosa la kuchana karatasi ya maelezo ya mpiga kura (Fomu namba moja) na mwingine kwa kosa la kujiandikisha mara mbili. Akizungumza juzi na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Juma Idd, kuhusu matukio hayo, yaliyotokea Jimbo la Arusha Mjini, alisema Fauzia Abdurai Mussa, ambaye ni binti aliyekuwa amevaa vazi maalumu la hijab alifika kujiandikisha fomu namba moja katika kituo cha YMCA kata ya Kati ambaye alipofika katika eneo la kupiga picha alitakiwa kuvua hijabu ili sura ionekane lakini alikataa. “Lakini huyu binti alipolazimishwa kuvua vazi hilo alikataa na kutoka nje, na alipofika nje alichana karatasi hiyo ambayo ndiyo fomu namba moja yenye maelezo yake na hapo alikamatwa na askari kutokana na uharibifu wa mali ya serikali na yupo ndani anasubiri kupelekwa mahakamani Jumatatu,” alisema. Mtuhumiwa wa pili aliyemtaja kuwa ni Daniel Leonard alikamatwa katika kituo cha shule ya msingi Daraja mbili, kata ya Daraja mbili baada ya kudaiwa kujiandikisha Julai 13 na Julai 15, mwaka huu katika kituo hicho, hivyo alitiwa mbaroni.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Diamond Platnumz Ashinda Tuzo ya BEST LIVE ACT Ya MTV MAMA………Orodha ya Washindi Wote Iko Hapa

$
0
0

Yako majina mawili yaliyoiwakilisha Tanzania kwenye Category 13 za MTV Africa Music Awards 2015, Diamond Platnumz na Vanessa Mdee ‘Vee Money’… Kura zimepigwa na usiku wa leo ndio ilikuwa fainali yenyewe ndani ya Durban South Africa ukumbi wa Durban International Convention Centre. Tanzania imetoka kifua mbele pia kwa mara nyingine, Daimond Platnumz kafanikiwa kupata ushindi wa Tuzo ya Best Live Act, ambapo alikuwa katika Category tatu tofauti na Vee Money alikuwa kwenye Category moja. List ya Washindi wote hii hapa.. Best Female: Yemi Alade (Nigeria) > > > Mshindi. Bucie (South Africa) Busiswa (South Africa) Seyi Shay (Nigeria) Vanessa Mdee (Tanzania) Best Male: Davido (Nigeria) > > > Mshindi AKA (South Africa) Diamond (Tanzania) Sarkodie (Ghana) Wizkid (Nigeria) Best Group: P Square (Nigeria) > > > Washindi. B4 (Angola) Beatenberg (South Africa) Black Motion (South Africa) Sauti Sol (Kenya) Best New Act Transformed by Absolut: Patoranking (Nigeria) > > > Mshindi. Anna Joyce (Angola) Cassper Nyovest (South Africa) Duncan (South Africa) Stonebwoy (Ghana) Best Hip Hop: Cassper Nyovest (South Africa) > > > Mshindi. K.O. (South Africa) Phyno (Nigeria) Olamide (Nigeria) Youssoupha (DRC) Best Collaboration: AKA, Burna Boy, Da LES & JR: “All Eyes On Me” (South Africa/ Nigeria) > > > Washindi. Davido featuring Uhuru & DJ Buckz: “The Sound” (Nigeria/SA) Diamond & Iyanya: “Bum Bum” (Kenya/Nigeria) Toofan & DJ Arafat: “Apero Remix” (Togo/Ivory Coast) Stanley Enow & Sarkodie: “Njama Njama Cow Remix” (Cameroon/Ghana) Song of the Year: Mavins: “Dorobucci” (Nigeria)> > > Washindi. Cassper Nyovest: “Doc Shebeleza” (South Africa) Euphonik featuring Mpumi: “Busa” (South Africa) DJ Fisherman & NaakMusiQ featuring DJ Tira, Danger & Dream Team: “Call Out” (South Africa) K.O featuring Kid X: “Caracara” (South Africa) Lil Kesh Featuring Olamide & Davido: “Shoki Remix” (Nigeria) Sauti Sol: “Sura Yako” (Kenya) Toofan: “Gweta” (Togo) Wizkid: “Show You The Money” (Nigeria) Yemi Alade: “Johnny” (Nigeria) Best Live: Diamond Platnumz (Tanzania) > > > Mshindi. Big Nuz (South Africa) Flavour (Nigeria) Mi Casa (South Africa) Toofan (Togo) Video of the Year: “Nafukwa” – Riky Rick; Director: Adriaan Louw > > > Mshindi. “Crazy” – Seyi Shay Featuring Wizkid; Director: Meji Alabi “Doors” – Prime Circle; Director: Ryan Kruger “Love You Everyday” – Bebe Cool; Director: Clarence Peters “The Sound” – Davido Featuring Uhuru & DJ Buckz; Director: Sesan Best Pop & Alternative: Jeremy Loops (South Africa) > > > Mshindi. Fuse ODG (Ghana) Jimmy Nevis (South Africa) Nneka (Nigeria) Prime Circle (South Africa) Best Francophone: DJ Arafat (Ivory Coast) > > > Mshindi. Jovi (Cameroon) Laurette Le Pearle (DRC) Tour 2 Garde (Ivory Coast) Toofan (Togo) Best Lusophone: Ary (Angola) > > > Mshindi B4 (Angola) Nelson Freitas (Cape Verde) NGA (Angola) Yuri Da Cunha (Angola) Personality of the Year: Trevor Noah (South Africa) > > > Mshindi. Basketmouth (Nigeria) Bonang Matheba (South Africa) OC Ukeje (Nigeria) Yaya Toure (Ivory Coast) MAMA Evolution (Category mpya): D’Banj (Nigeria) > > > > Mshindi. Best International: Nicki Minaj (Mshindi) Artist of the Decade: P Square (Washindi) MTV Base Leadership Award: Saran Kaba Jones & S’Bu Mavundla (Washindi)

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Shilole na Nuh Mziwanda Wapigana Chini……….Mziwanda Amwita Shilole ASHA NGEDERE

$
0
0

Ile couple ya wasanii wa kibongo wasioishiwa skendo, Shilole na Nuh Mziwanda imeubuka upya kwa staili ya kipekee. Tumezoea kusikia Shilole kamnasa makofi Mziwanda, mara kampiga chupa na mengine mengi ya aina hiyo. Awamu hii wamekuja na mpya ya kuchambana live mitandaoni. Nuh kafananishwa na ganda la ndizi huku Shilole akifananishwa na Asha Ngedele…… Aliyelianzisha Varangati hili ni Shilole, ambaye ameandika ujumbe huu instagram. “Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika’ila sasa kama gari limewaka’aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na maisha yangu’Mimi na yeye baaaaaaasi #GaNdALaNdiZi .™@shilolekiuno” Nuhu nae akaona isiwe tabu akamwaga ugali, na kachumbari “Mwanaume wa kweli ukaa kimya’sibishani na upumbavu’mwanamke asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa’na kuvumilia mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu’familia na’wasanii wenzangu na wadau’anaanza kunitukana mitandaoni for whaaaat!!! Mxeeeeew’mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu na mtu atakae thamini moyo wangu ‘nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari ‘mimi nacheka tu #AsHaNgeDerE. ™@mziwandanation”

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Benard Membe Atangaza Kuachana Na Siasa…….Asema Hatagombea Wadhifa Wowote Mwaka Huu

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe, amesema hatogombea wadhifa wowote kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba anapanga kujishughulisha na masuala yake ya kibinafsi. Membe ambaye alikuwa akitafuta tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania urais mwezi Oktoba lakini akashindwa kufikia lengo hilo, amesema kuwa, hatotafuta nafasi ya ubunge katika jimbo lake la Mtama. Hata hivyo amesema ataendelea kukiunga mkono chama chake cha CCM na atampigia debe mgombea urais aliyeteuliwa na chama hicho, Bw. John Magufuli. Awali kulikuwa na tetesi kwamba Membe angegombea ubunge baada ya kukosa nafasi ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM. Huku hayo yakijiri, chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kupata pigo baada ya baadhi ya wabunge wake kutangaza kuwa hawatogombea tena nafasi zao kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao. Tayari madiwani 20 wa CCM katika jimbo la Monduli wametangaza kuhamia Chadema na kumtaka mbunge wao, Edward Lowassa kufuata mkondo huo.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CCM, Ester Bulaya Amekataa Kuchukua Fomu ya Ubunge kwa tiketi ya CCM.

$
0
0

Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya, kutangaza kukitosa kwa kutangaza uamuzi wake wa kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho. Bulaya ambaye alikuwa mbunge machachari kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni , ametangaza kutogombea ubunge kupitia CCM wakati akizungumza na mtandao huu baada ya kazi ya kuchukua fomu ndani ya chama hicho na kurejesha kuhitimishwa rasmi nchini jana. Tangu mwanzo mwa mwaka huu, Bulaya alitangaza kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda kupambana na Mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. Bulaya amekuwa kada wa pili ambaye alikuwa mbunge kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mbunge wa kwanza kutangaza kutogombea ubunge kupitia CCM baada ya James Lembeli, ambaye alikuwa Mbunge wa Kahama. Hata hivyo, Bulaya hakuweka wazi kama ana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na kutimiza azma yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Ingawa Bulaya hajaweka wazi, vyama ambavyo vimekuwa vikitajwa kusubiri makada kutoka CCM kujiunga navyo ili wawanie ubunge ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (Cuf). Mwenyekiti Monduli Apigilia Msumari Wakati ikiwa hivyo kwa Bulaya, hali bado si shwari ndani ya CCM Wilaya ya Monduli baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Edward Sapunyo, Kupigilia msumari wa mwisho na kubariki hatua ya madiwani wake 20 kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza mjini hapa jana, Sapunyo ambaye alikuwa Diwani wa kata ya Moita, alisema madiwani wake hawawezi kusubiri hadi Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, atoe kauli kuhusu hatma yake ya kisiasa ndani ya CCM. Kauli ya Sapunyo ambaye hatagombea udiwani uchaguzi wa mwaka huu, imekuja siku moja baada ya madiwani 20 wa jimbo hilo kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). “Hatuwezi kuona baba yetu anapigwa na kuanguka chini halafu tusubiri kauli yake, ni lazima tuchukue hatua mara moja…hii haivumiliki, kitendo alichofanyiwa (Lowassa) na vikao vya CCM mjini Dodoma hivi karibuni kwa kukata jina lake pasipo kumpa haki ya kumsikiliza siyo cha kidemokrasia,” alisema. Lowassa na makada wenzake wa CCM 38 walichukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu. Katika kinyanyang’anyiro hicho, jina la Lowassa na wenzake yalikatwa katika hatua ya mwanzo, hali ambayo imezua malalamiko kwamba ikidaiwa kuwa hawakupewa nafasi ya kuhojiwa. “Tumepigwa, tumesambaratika (CCM) Monduli, hatuwezi kuchukua fomu za kuomba kugombea au kutetea nafasi zetu ndani ya chama hiki, tumehamia Chadema,” alisema. Akizungumzia hali ilivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alidai kuwa siyo kweli kwamba madiwani wote wamekihama chama chao. Kimaro alidai kuwa baadhi ya madiwani waliotangaza kukihama chama hicho wameanza kusalitiana. Alisema madiwani hao ambao anawaita ni makada baada ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Monduli kuvunjwa, walifanya mkutano kwa kushawishiwa na mmoja wao. Alisema ushawishi huo unatokana na uchu wa madaraka alionao kwa kuwa tayari wananchi wa Jimbo la Monduli, wanapenda aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM, Namelok Sokoine, kuchukua fomu za ubunge wa jimbo hilo. Alisema kutokana na ugumu huo, diwani huyo wa zamani ametumia mbinu ya kuwarubuni wenzake wakihame chama hicho ili agombea ubunge kwa tiketi ya Chadema. “Huo ni uchu wa madaraka aliyo nayo,” alisema na kuongeza: “Diwani huyo hakubaliki na wananchi wa kata yake.” Alidai kabla ya kutangaza kukihakama chama hicho, madiwani hao walikuwa wameshafanya kikao na kuweka azimio la pamoja la kuondoka CCM, lakini juzi walipotangaza uamuzi wao, walijikuta wapo madiwani watatu. Alisema baadhi ya madiwani walimfuata ofisini kwa lengo la kumuomba radhi lakini yeye aliwaambia waende kuwaomba radhi wananchi katika kata zao. “Madiwani wachache walikuja hapa ofisini kuomba radhi kwa Katibu wa CCM Wilaya, nikawaambia waende kuwaomba radhi wananchi,” alisema. Akimzungumzia Lowassa, alisema anachoelewa ni kwamba hajatoa tamko lolote kama anakihama chama hicho kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na mitandao ya kijamii. “Bado tuna imani na Lowassa kuwa ni CCM, mpaka sasa hajatoa tamko lolote kukihama chama, lakini ikiwa vinginevyo itakuwa hatari kubwa,” alisema.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Lupumba Aiyumbisha UKAWA

$
0
0

Wakati bado haijafahamika lini mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) atatangazwa rasmi, imefahamika kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Profesa Ibrahim Lipumba, amekuwa ndiyo kikwazo cha kutopatikana kwa mgombea huyo. Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu kwa siku nne sasa umebaini kuwa hatua ya Profesa Lipumba kukwepa vikao vya Ukawa, ni mkakati mahsusi unaolenga kukwamisha mchakato wa kupatikana mgombea urais wa umoja huo. Ukawa unaundwa na Cuf, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi na NLD. Taarifa kutoka ndani ya vikao vya Ukawa vimeeleza kuwa kikao cha kwanza cha umoja huo, Profesa Lipumba aliulizwa kwanini anataka kugombea urais na kujibu kuwa anaamini kuwa yeye ndiye bora kuliko wengine. Hata hivyo, alipoulizwa kama amejiandaa vipi kirasilimali iwapo atateuliwa kuwania nafasi hiyo kupitia Ukawa, hakuwa na majibu ya kujitosheleza na badala yake ilibainika kuwa Cuf imejiandaa zaidi Zanzibar kuliko Tanzania Bara. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Profesa Lipumba amekuwa aking’ang’ania agombee urais na hata mkutano wa mwisho wa Ukawa ambao hakuhudhuria, inadaiwa kwamba ni mkakati wa kushinikiza ateuliwe yeye kugombea nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi. Katika vikao vya Ukawa, hoja kubwa imekuwa ni suala la mgombea urais, nafasi ambayo inawaniwa na Profesa Lipumba ambaye tayari ameshachukua fomu kupitia chama chake cha Cuf pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, anayeungwa mkono na vyama vyote vinne. Profesa Lipumba ameshagombea urais mara nne bila mafanikio, wakati Dk. Slaa aligombea mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili, akiwa ameitikisa CCM iliyopoteza asilimia takriban 20 ya kura za mwaka 2005. Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, akizungumza na waandishi wa habari Julai 14, mwaka huu, alisema umoja huo utamtangaza mgombea wao wa urais baada ya siku saba ambazo zinaisha wiki hii. Alisema wamekubaliana kutangaza mgombea baada ya siku saba ili kutoa nafasi kwa viongozi walioshiriki majadaliano hayo kutoa taarifa kwa wanachama wa vyama vyao juu ya mambo waliokubaliana. Aidha, Mbatia alikanusha uvumi kuwa kada wa CCM na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ana mpango wa kujiunga na umoja huo ili apewe nafasi ya kugombea urais baada ya kukosa nafasi hiyo kupitia chama chake. Mbatia pia alikanusha uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna mvutano mkubwa ndani ya Ukawa katika suala la mgombea urais ambao umesababisha Cuf kutaka kujitoa. “Hakuna ukweli katika hilo na hata leo (jana), nimeongea na Profesa Lipumba kumtaarifu hatua tulioyofikia, hivyo hakuna mpasuko wowote,” alisema Mbatia. Kabla ya taarifa hiyo ya Mbatia,Ijumaa iliyopita Ukawa walitoa taarifa ya kwamba wangemtangaza mgombea wake ndani ya saa 24, ahadi ambayo haikutimizwa.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Chadema yatangaza ratiba kura ya maoni.

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza ratiba ya kuanza kura ya maoni ndani ya chama hicho kuwa itaanza leo (Julai 20) na kumalizika Julai 25 mwaka huu. Kura hiyo inakuja baada ya kukamilika kwa kazi ya uchukuaji fomu za kuomba kuwania ubunge na udiwani, ndani ya chama hicho. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene, alisema jana kuwa katika hatua hiyo, kila uongozi wa kanda umepanga ratiba yake ya kura za maoni katika majimbo mbalimbali. Makene alisema kupitia mchakato huo wa kura ya maoni, wana wa Chadema watapata wagombea ubunge makini ambao watakihakikishia chama ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu, utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Alisema ili kufanikisha mchakato huo, Waratibu wa Kanda za Chama, Makatibu wa Mikoa na Makatibu wa Majimbo watoe ushirikiano kwa vyombo vya habari ili viweze kufuatilia nchi nzima na kuuhabarisha umma wa Watanzania. Mnyika achukua fomu ya Ubunge Wakati huo huo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (pichani), jana alichukuliwa fomu na Wazee wa chama hicho wa jimbo hilo wakimshinikiza kuwania tena nafasi hiyo. Wazee hao ambao walifika kwenye ofisi za jimbo maeneo ya Kimara Kona, majira ya mchana walimtaka kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine. Akizungumza na mtandao huu, Katibu wa jimbo hilo, Justine Mollel, alisema katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Ubunge kwenye jimbo hilo hadi jana aliyechukua fomu ni Mnyika pekee. Alieleza kuwa, kwenye jimbo jipya la Kibamba jumla ya makada saba wa Chadema, walijitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo. “Ni kweli Mnyika leo amechukuliwa fomu na Wazee wa Chadema Jimbo la Ubungo kwa ajili ya kuwania nafasi ya Ubunge na mipaka sasa hakuna aliyechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo na anatarajia kuirudisha leo jioni (jana),” alisema Mollel.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Upinzani waja juu Magufuli kutumia ndege ya Serikali

$
0
0

Wanasiasa wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kutumia ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa. Dk Magufuli, juzi alikwenda Mwanza kwa ziara maalumu ya kujitambulisha akitumia ndege ya Serikali aina ya Fokker F28, jambo ambalo limeibua hisia tofauti. Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki alisema kitendo cha CCM kutumia ndege ya Serikali hakivunji sheria na taratibu zozote kwa kuwa mbali na kusafirisha viongozi wa Serikali, pia wanaruhusiwa kufanya biashara kwa kuhudumia umma. Pia, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema walifuata taratibu zote kuikodi ndege hiyo na kwamba chama chake ni kikubwa na hakiwezi kushindwa kukodi usafiri huo. “Ile ni ndege ya Serikali, yeyote anayetaka kuitumia aende kulipia tu, atapewa. Sisi tumekwenda kama wateja wa kawaida tukalipia, ukitaka kujua ni kiasi gani kawaulize wahusika watakueleza,” alisema Nape. Kuhusu suala hilo la gharama, Kapteni Mhaiki alisema gharama ya kukodi ndege hizo zipo tofauti kutokana na aina inayohitajika akisema aliyoitumia Dk Magufuli inagharimu Dola za Marekani 4,000 sawa na Sh8.4milioni kwa saa moja. Akizungumzia suala hilo jana, Kiongozi wa chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe alisema viongozi wa Serikali wamekuwa na utamaduni wa kutumia mali za umma kwa shughuli za kisiasa na kusahau kwamba rasilimali hizo ni za Watanzania wote bila kujali itikadi zao. Zitto na Mbowe Zitto alisema jambo hilo halijaanzia kwenye ziara ya Dk Magufuli, bali hata mawaziri wote waliochukua fomu walitumia magari ya Serikali kuzunguka nchi nzima kutafuta wadhamini wao kwa nafasi ya urais. “Jambo hili si kwa CCM pekee, tunaona pia gari la Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), likitumika kwenye mikutano yake ya kichama. Lile ni gari la Serikali; kwa hiyo lazima tuupige vita utamaduni huu,” alisema Zitto. Alisema CCM ina wajibu wa kuwaeleza Watanzania sababu za kutumia ndege ya Serikali na kama wamelipia fedha ni kiasi gani kilicholipwa huku akisisitiza kuwa utamaduni huu uliokithiri unaligharimu Taifa. “Mali za umma lazima zitumike kwa shughuli za Serikali na siyo shughuli za kichama. Hili halina upinzani wala CCM, ni jambo linalotakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote ili rasilimali zetu zitumike ipasavyo,” alisisitiza kiongozi huyo. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema limekuwa ni jambo la kawaida kwa CCM kutumia vyombo vya Dola katika kufanikisha mambo yao na kwamba sababu za kwamba ndege za Serikali zipo wazi kwa umma ni ‘danganya toto’ ili kufurahisha wananchi. “Eti ndege hizo zinaweza kukodiwa na mtu binafsi au chama, nani kakwambia? Nenda kakodi kama utapata. Ukweli ni kwamba Magufuli hakuikodi hiyo ndege, kama ni kweli wamekodi watuonyeshe walilipaje?” alihoji Mbowe na kuongeza. “Chadema haijawahi kwenda kukodi kwa sababu ina uhakika haitaipata, hasa ikizingatiwa “viwanja tu vya michezo vinavyomilikiwa na CCM havijawahi kutolewa vitumike kwa mikutano ya upinzani tangu mfumo wa vyama vingi uanze zaidi ya miaka 20 iliyopita.” Mwenyekiti huyo wa Chadema, alisema hata polisi, mahakama na vyombo vya habari vya Serikali vimekuwa vikitumika vibaya kuilinda CCM iendelee kukaa madarakani. Alipoulizwa juu ya gari la Serikali analotumia kuonekana kwenye mikutano yake ya kisiasa alijibu: “Nilipopewa gari na Serikali lilikuwa ni kwa matumizi ya upinzani, mikutano ya kisiasa ninayohudhuria ni sehemu ya kazi za upinzani… sasa wanaohoji walitegemea nitalitumia gari hilo kwa ajili ya Serikali? Nenda kawaambie habari ndiyo hiyo na Bunge likivunjwa nitalirudisha.” Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK), Constatine Akitanda alisema ana shaka kubwa iwapo ndege hiyo ilikodiwa na CCM na kulipiwa gharama zinazotakiwa. “Sisi tuna uhakika gani kuwa CCM walikodi? Hata hizo fedha tukisema twende tukaangalie je, ni kweli wamelipa au wamechukua tu hiyo ndege?… hata ukisema tukafanye ‘auditing’ (ukaguzi) hutakuta kitu pale,” alisema Akitanda. Ufafanuzi wa wakala Katika ufafanuzi wake, Kapteni Mhaiki alisema hakuna haja ya suala hilo kuchukuliwa kisiasa… “Jukumu la kwanza ni kubeba viongozi wa Serikali lakini kama kuna muda wa ziada tunawahudumia watu wengine kibiashara na huwa tunasafirisha hata timu za mpira na wageni kutoka nje ya nchi wanapotembelea nchini. “Mtu yeyote anaruhusiwa kuomba kuikodi, atapatiwa ankara yake… hata awe CUF, Chadema au chama chochote kile kama kuna nafasi anapata,” alisema. Alipoulizwa juu ya tuhuma za upendeleo kwa chama tawala hivyo kutoleta uwanja sawa wa ushindani, alijibu: “Upendeleo upi unaozungumza au unautaka? Hata wewe mwandishi ukitaka tupigie simu ndege ikiwapo utapata.” TGFA kwa sasa ina ndege nne ambazo ni Fokker F28 ya mwaka 1978 yenye usajili wa 5H-CCM, Piper PA-31 Navajo (1980, 5H-ILS), Fokker 50 (1992, 5H-TFG) na Gulfstream 550 ya mwaka 2004 iliyosajiliwa kwa namba 5H-ONE. Kama mwaka 2010 Sakata la matumizi ya ndege ya Serikali lilishawahi kujitokeza mwaka 2010 wakati wa kampeni baada ya kumbeba mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma. Kitendo hicho kilimfanya aliyekuwa Meneja wa Kampeni kipindi hicho ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuonyesha risiti zilizotumika kulipia huduma za ndege hizo.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Solar Hot Water Panel Differential Pump Controller

$
0
0

This circuit optimises the circulation of heated water from solar hot water panels to a storage cylinder. It achieves this by controlling a 12V DC pump, which is switched on at a preset temperature differential of 8°C and off at about 4°C. This method of control has distinct advantages over some systems that run the pump until the differential approaches 0°C. In such systems, the pump typically runs whenever the sun shines. A small 10W solar panel charging a 12V SLA battery is sufficient to run the controller. Most commercial designs use 230VAC pumps, which of course don’t work when there is a power outage or there is no AC power at the site. Operation: Temperature sensors TS1 & TS2 are positioned to measure the highest and lowest water temperatures, with one at the panel outlet and the other at the base of the storage cylinder. The difference between the sensor outputs is amplified by op amp IC1d, which is configured for a voltage gain of about 47. As the sensors produce 10mV/°C, a difference of 8°C will produce about 3.76V at the op amp’s output (pin 14). The output from IC1d is fed into the non-inverting input (pin 10) of a second op amp stage (IC1c), which is wired as a voltage comparator. The op amp’s inverting input (pin 9) is tied to a reference voltage, which can be varied by trimpot VR3. When the voltage from IC1d exceeds the reference voltage, the output of the comparator (pin 8) swings towards the positive rail. A 10MW resistor feeds a small portion of the output signal back to the non-inverting input, adding some hysteresis to the circuit to ensure positive switching action. A third op amp stage (IC1b) acts as a unity-gain buffer. When the comparator’s output goes high, the buffer stage switches the Mosfet (Q1) on, which in turn energises the pump motor. Mosfet Q1’s low drain-source on-state resistance means that in most cases, it won’t need to be mounted on a heatsink. The prototype uses a Davies Craig EBP 12V magnetic drive pump, which draws about 1A when running and is suitable for low-pressure hot water systems only (don’t use it for mains-pressure systems as it may burst!). For mains-pressure systems, the author suggests the SID 10 range of brass-body magnetic drive pumps from Ivan Labs USA. Circuit diagram: Solar Hot Water Panel Differential Pump Controller Circuit Diagram Setup: Each LM335 temperature sensor and its associated trimpot is glued to a small copper strip using high-temperature epoxy. It is then waterproofed with silicon sealant and encapsulated in heatshrink tubing. Standard twin-core shielded microphone cable can be used for the connection to the circuit board. Before sealing the two units, adjust their trimpots to get 2.98V at 25°C [(ambient temperature x .01) + 2.73V] between the “+” and “-” terminals. When both have been adjusted, clamp them together and allow their temperatures to stabilise for a few minutes. Next, measure the output voltage from the differential amplifier (IC1d), which should be close to 0V. If not, tweak one of the pots until it is. Separate the two and warm the panel sensor (TS1), monitoring the output of IC1d. You should see a marked increase in voltage, remembering that an 8°C difference between the sensors should give an output of about 3.76V. The pump switch-on point is set by VR3 and can be adjusted over a practical range of about 4-10°C differential (1.88-4.70V). Adjust VR3 to get about 3.8V on pin 9 of IC1c as a starting point. If set too low and the panels are located far from the cylinder, much of the heat will be lost in the copper connecting pipes. On the other hand, if set too high and the weather is mostly cloudy, then the pump will not switch on very often, as the panels will not get hot enough. For best results, use copper pipes for the panel plumbing and insulate them with tubes of closed-cell foam. As the pipes cool down between pump operations, small diameter pipes of 15mm are more efficient than larger sizes as they contain less static water. In practice, the pump in the author’s setup switches on for about 30 seconds every 4-5 minutes. As the Davies pump shifts 13 litres/minute, it displaces the heated water from a single panel in about 14 seconds. There is a thermal lag in the sensor readings, so after the pump stops, the temperature difference will keep decreasing for 40 seconds or so as the panel sensor cools down and the cylinder sensor heats up.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Pump Controller For Solar Hot Water System

$
0
0

This circuit optimises the operation of a solar hot water system. When the water in the solar collector is hotter than the storage tank, the pump runs. The circuit comprises two LM335Z temperature sensors , a comparator and Mosfet. Sensor 1 connects to the solar collector panel while Sensor 2 connects to the hot water panel. Each sensor includes a trimpot to allow adjustment of the output level. In practice, VR1 and VR2 are adjusted so that both Sensor 1 and Sensor 2 have the same output voltage when they are at the same temperature. The Sensor outputs are monitored using comparator IC1. When Sensor 1 produces a higher voltage than Sensor 2, which means that sensor 1 is at a higher temperature, pin 1 of IC1 goes high and drives the gate of Mosfet Q1. This in turn drives the pump motor. IC1 includes hysteresis so that the output does not oscillate when both sensors are producing a similar voltage. Hysteresis comprises the 1MO feedback resistor between output pin 1 and non-inverting input pin 3 and the input 1kO resistor. This provides a nominal 12mV hysteresis so that voltage at Sensor 1 or Sensor 2 must differ by 12mV for changes in the comparator output to occur. Circuit diagram : Since the outputs of Sensor 1 and Sensor 2 change by about 10mV/°C, we could say that there is a degree of hysteresis in the comparator. Note that IC1 is a dual comparator with the second unit unused. Its inputs are tied to ground and pin 2 of IC1 respectively. This sets the pin 7 output high. Since the output is an open collector, it will be at a high impedance. Mosfet Q1 is rated at 60A and 60V and is suitable for driving inductive loads due to its avalanche suppression capability. This clamps any inductively induced voltages exceeding the voltage rating of the Mosfet. The sensors are adjusted initially with both measuring the same temperature. This can be done at room temperature; adjust the trimpots so that the voltage between ground and the positive terminal reads the same for both sensors. If you wish, the sensors can be set to 10mV/°C change with the output referred to the Kelvin scale which is 273K at 0°C. So at 25°C, the sensor output should be set to (273 + 25 = 298) x 10mV or 2.98V. Note: The sensors will produce incorrect outputs if their leads are exposed to moisture and they should be protected with some neutral cure silicone sealant. The sensors can be mounted by clamping them directly to the outside surface of the solar collector and on an uninsulated section of the storage tank. The thermostat housing is usually a good position on the storage tank.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Breaking News kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar kuhusu Silaha zilizoibiwa Kituo cha Polisi Stakishari..

$
0
0

Kwenye mfululizo wa matukio yaliyoshtua watu wengi Tanzania, liko pia ambalo lilitokea usiku wa July 12 2015 ambapo Majambazi walivamia  Kituo cha Polisi Stakishari Ukonga Dar , wakauawa watu 7 wakiwemo pia Askari wanne na watu wengine watatu. Leo taarifa imetolewa na Kamanda  Suleiman Kova  kwamba kuna watu watano wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo na pia kuna silaha ambazo zimekamatwa, ziko Bunduki 15 pamoja na Risasi 28 ambazo zote ni sehemu ya zilizoibiwa wakati wa tukio la Ujambazi uliofanyika Stakishari.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

KTM and Piaggio Receive Funding From EU to develop ELV

Suzuki Files Patent For Hybrid Motorcycle 

Build a Solar Garden Light Circuit Diagram

$
0
0

 This is a Solar Garden Light Circuit Diagram that consists of a very simple system garden lighting that can be done by using some common electronic parts and a small solar panel. The electronic design is simple yet very efficient, has the advantage of being solar powered, it requires only one transistor, one 2.5 volt solar panel and some other common electronic components you can remove junk.  This solar lighting system automatically turns on the LEDs when the solar panel detects no light turns off when the solar panel produces more than 1v and charges the battery when the panel produces more than 2.1V The coils in this circuit require a core material F29 and they must be made with wire of 0.095 mm in core 2.6x6mm. “This circuit uses the system joule thief (joule thief) to provide voltage necessary for the LED, so other coils can be tested. Solar Garden Light Circuit Diagram

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Simple Solar Engine Circuit Diagram

$
0
0

  Simple Solar Engine Circuit Diagram Small DC motor runs off of calculator solar cell in dim light . How do we achive 10nA operation? By using diodes in place of pull up resistors, and by isolating the DC load from the trigger circuit via junction drops and the 10nF capacitor. If there is too much power comming from the solar cell then the motor might run too often or even continuously. You can avoid this by putting a 100K ohm resistor in series with the solar cell.   Simple Solar Engine Circuit Diagram

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Viewing all 2247 articles
Browse latest View live