Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Museveni ndiye mshindi wa uchaguzi wa Uraisi Nchini Uganda,

$
0
0

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.    Rais Museveni amepata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.   Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye amepata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.   Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.   Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles