Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu inayofahamika kama Junior National Basket Association (JR.NBA), ufunguzi ambao umefanyika jijini Dar es Salaam. Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya mitoano Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana, katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,jana jijini Dar es Salaam. Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),jana jijini Dar es Salaam. Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, jana jijini Dar es Salaam. Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, jana jijini Dar es Salaam Sehemu ya mashabiki wa Mpira wa kikapu walio fika katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,jana jijini Dar es Salaam.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat