Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Wabunge 35 wa UKAWA Wafukuzwa Bungeni

$
0
0

Wabunge  35 wa kambi ya upinzani bungeni jana walitolewa nje ya ukumbi wa bunge na spika wa bunge  Anne Makinda na kupewa adhabu ya  kutokuhudhuria vikao vitano kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge .   Mara baada ya kikao cha bunge kuanza spika wa bunge alinza kwa kuwakumbusha wabunge namna ya kufuata kanuni hasa pale wanapotaka kuondoa muswada wowote.   Hali ilibadilika ghafla Bungeni baada ya Mbunge Ezekiel Wenje kuomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao? Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… ndipo spika aliamua  kuwatoa nje.   Hata hivyo baada ya vurugu zote kuisha miswada yote mitatu ambayo ni  ya sheria ya petroli, sheria ya usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi pamoja na sheria ya uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uchimbaji Tanzania iliwasilishwa Bungeni.   Majina ya Wabunge waliotimuliwa  ni, Ezekiel Wenje Mussa Kombo Masoud Abdallah Salim Rebecca Ngodo Sabrina Sungura Khatib Said Haji Dr. Anthony Mbassa Maulidah Anna Valerian Komu Kulikoyela Kahigi Cecilia Pareso  Joyce Mukya Mariam Msabaha  Grace Kiwelu Israel Natse   Mustapha Akonaay Konchesta Rwamlaza Suleiman Bungura  Rashid Ali Abdallah  Ali Hamad Riziki Juma Rukia Kassim Ahmed Azza Hamad Khatibu Said Haji Kombo Khamis Kombo Ali Khamis Seif Haroub Mohammed Shamisi  Kuruthum Jumanne Mchuchuli Amina Mwidau Mkiwa Kimwanga Salum Baruhani  Marry Stellah Malaki Rashid Ally Omary Mwanamrisho Abama Lucy Owenya FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles