Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

KIKWETE: Hakuna Mtanzania Aliyekufa kwa Njaa

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa hakuna mtanzania aliyewahi kufa njaa kwani nchi haikuwahi kuwa na upungufu wa chakula na kusababisha hali ya kuleta athari za kifo kutokana na njaa kwa wananchi wake. Dkt. Kikwete aliyasema hayo jana mjini Lindi wakati akiwahutubia watanzania katika maadhimisho ya kitaifa ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika mkoani humo Dkt. Kikwete alisema kinachofanyika sasa ni kuhakikisha wakulima wanalima mazao mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuwatafutia masoko zaidi ya ndani na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya kilimo kwa kukuza uchumi na kuwaondolea watanzania Umasikini. Aliongeza kuwa licha ya Uzalishaji kuongezeka lakini bado Serikali haijafika inapopataka hivyo haina bundi kuongeza juhudi zaidi ili kuendelea sekta ya kilomo iwe yenye tija zaidi. Katika maadhimisho hayo Dkt. Kikwete alitumia nafasi yake kuwaaga wakulima ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza muda wake madarakani, huku akiwataka watanzania kutumia vyema haki yao ya kupiga kura na kumchagua kiongozi wanaempenda

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles