Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Majenerali 2 waihama kambi ya Machar

$
0
0

Sudan Kusini Majenerali wawili waasi nchini Sudan Kusini wametangaza kwamba wamejitenga na kundi la waasi linaloongozwa na Riek Machar. Gathoth Gatkuoth na Peter Gadet wamesema kuwa sasa wanakabiliana na waasi hao pamoja na serikali mjini Juba. Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini vilizuka mwaka 2013 kati ya vikosi vilivyo vitiifu kwa rais Salva Kiir na wapiganaji wa Machar aliyekuwa naibu wake. Gathoth Wapatanishi wa eneo hili wameweka makataa ya tarehe 17 mwezi Agosti kwa makubaliano ya amani kuafikiwa. Haijulikani waasi hao wana wanajeshi wangapi,lakini wachanganuzi wanasema kuwa majenerali wote wawili wamekuwa na uwezo mkubwa ardhini na kujiondoa kwao kunaweza kuathiri pakubwa mazungumzo ya amani.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Latest Images

Trending Articles



Latest Images