Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Mtoto aliyekamatwa na saa wakidhani ni bomu amekaribishwa Ikulu ya Obama.. Mipango ya shule?

$
0
0

Unamkumbuka  Ahmed Mohamed  mtoto kutoka  Dallas, Texas   Marekani  aliyekamatwa na polisi baada ya kupeleka shule saa iliyodhaniwa kuwa ni bomu? Yes,  Ahmed  aliweka headlines nyingi sana  Marekani   na saa yake ambayo baadaye ilikuja kuonekana kuwa saa ile ilikuwa haina madhara yoyote kitendo ambacho pia kilisababisha mshituko mkubwa sana kwa mtoto huyo. Ahmed Mohamed . Headlines za  Ahmed  leo zipo tofauti sana, siku ya jumanne  October 20  familia ya Ahmed  ilitangaza maamuzi yao ya kuhamia  Doha ,  Qatar  baada ya taasisi inayoitwa ‘Qatar Foundation’   kutoa ofa ya kumlipia mtoto huyo malipo yote ya elimu yake ya sekondari mpaka degree yake ya kwanza! Kwenye mazungumzo na waandishi wa habari nchini  Marekani , familia ya  Ahmed  ilisema kwamba walipokea ofa nyingi sana za msaada baada ya stori ya  Ahmed   kuwafikia watu wa sehemu mbalimbali duniani na waliongeza kwa kusema kuwa wameamua kuchagua kwenda  Doha ,  Qatar  kwasababu wamefanya utafiti wao kama familia na wamegundua kuwa taasisi ya  ‘Qatar Foundation’   ina histori nzuri ya kuwajenga vijana wadogo kwa kukuza utamaduni wa uvumbuzi na ubunifu. Jana Ahmed alikutana na Rais Barrack Obama kwa mara ya kwanza Whitehouse kuzungumza na kuagana. > > >   ” Tunakamilisha mpango wa kuhamia Doha, Qatar ndani ya siku chache zijazo, tumepokea ofa nyingi juu ya Ahmed baada ya watu wengi kuguswa na stori yake lakini kama familia tumeona Ahmed atakuwa na fursa nzuri zaidi akiwa Qatar kwani Qatar Foundation inatoa mchango mkubwa kwenye kukuza utamaduni wa ubunifu na uvumbuzi kwa vijana wadogo kama Ahmed…”  

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles