Magufuli Apata Mapokezi ya Kutisha Kibaigwa
Esta Bulaya ni Moto wa Kuoteka Mbali……..Apata mapokezi ya kishindo Bunda, Amchamba na Kumlipua Wassira
ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Mara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi.Esta Bulaya ambaye juzi alitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amepata mapokezi makubwa Mjini Bunda jana akitokea jijini Mwanza akiwa na viongozi wa CHADEMA mkoani humo na Kanda ya Ziwa. Akiwahutubia wananchi katika Viwanja vya Stendi ya Zamani, Bi.Bulaya aliwapongeza wananchi kwa mapokezi makubwa waliyompa na kumlipua mbunge wa jimbo hilo aliyemaliza muda wake, Bw. Stephen Wassira akisema muda wake wa kukaa serikalini unatosha. Alisema katika Serikali ya Awamu ya Tano, viongozi kama Bw. Wassira hawafai kwani amekuwa Waziri muda mrefu lakini jimbo hilo bado halina maendeleo yaliyotarajiwa na wananchi. “Wazazi wangu mimi ni mwanachama wa CCM na mimi nimekulia ndani ya chama hicho hivyo mkiona nimekimbia, mjue mambo yamenifika shingoni, katika mkoa huu kuna rasilimali nyingi ambazo hazijatumika vizuri ili ziwaondolee wananchi umaskini,” alisema. Akizungumzia uwazi na uwajibikaji, alisema viongozi wengi wa CCM hawataki kuwatetea wananchi na kushindwa kuwasimamia watendaji wa Serikali akitolea mfano mradi mkubwa wa maji mjini humo ambao umechukua miaka tisa bila Bw.Wassira kuukamilisha. “Leo hii Wassira atakuja na sera gani kwa wananchi wakati ameshindwa kutekeleza wajibu wake kama mbunge na kiongozi wa Serikali, tuwakatae viongozi wa ngazi zote wanaotokana na CCM,” alisema. Aliongeza kuwa, umefika wakati wa majimbo yote mkoani humo kuchukuliwa na wagombea wa CHADEMA ambao watatimiza ahadi zao kwa wananchi na kutatua kero walizonazo. Bi.Bulaya aliweka wazi dhamira yake ya kuwania ubunge wa Bunda Mjini kwa tiketi ya CHADEMA ambapo leo atashiriki kura ya maoni ya kumpata mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA. Naye mbunge wa Kahama, Bw. James Lembeli, alidai kuchoshwa na ufisadi uliopo ndani ya CCM na kuwataka wananchi wakubali kuiunga mkono CHADEMA kwa kuwaweka madarakani na kushika dola katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Mbunge wa Musoma Mjini, Bw. Vicent Nyerere, alilitaka Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano katika Uchaguzi Mkuu na kuacha kuitetea CCM huku akidai jeshi hilo ni sehemu ya Watanzania ambao wote wamepigika.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Rushwa yaahirisha kura ya maoni Chadema
Uchaguzi wa kura za maoni ndani ya Chadema katika Jimbo la Bariadi umeahirishwa baada ya kubainika kwa matukio yanayoashiria vitendo vya rushwa. Wakizungumza baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya walisema hawataki kuingiliwa na virusi vya rushwa ndani ya chama hicho, kwa kuwa hali hiyo italeta mpasuko na makundi. Wajumbe hao wameutaka uongozi Chadema kuwa makini na wanachama mamluki wanaohama kutoka vyama vingine vya upinzani ili wasikivuruge. “Hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi inaonyesha ni namna gani chama kilivyo makini ili wanaotoa rushwa wajifunze umakini huu na wananchi waelewe kuwa chama kinatetea wanyonge,” alisema Makula Saguda. Hata hivyo, mjumbe mwingine, Masanja Lujani alipinga hatua hiyo akisema kuahirishwa uchaguzi ni ubadhilifu ambao haufai akisisitiza kuwa kama wamekamata mtu akiwa anagawa rushwa wangemtoa katika uchaguzi na wengine wakaendelea. Msimamizi wa uchaguzi huo, Emmanuel Mbise alisema uchaguzi huo umeahirishwa baada ya kukamata watu wakigawa rushwa kwa baadhi ya wagombea. “Chadema kinaaminiwa na kinapendwa na watu kwa sababu hakikubaliani na rushwa, kwa mujibu wa katiba na mamlaka niliyopewa, nimeamua kuahirisha uchaguzi hadi utakapotangazwa tena kutokana na uchaguzi huu kutawaliwa na rushwa,” alisema Mbise. Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Simiyu, Wilson Mshuda ambaye pia ni mgombea katika jimbo hilo alisema: “Hatuwezi kunyamaza kimya, hata katiba ya chama kuanzia u kurasa wa 86 inaongelea mgombea ambaye ataonekana kutoa rushwa kwa wajumbe kuwa atakuwa amejiondoa katika kinyang’anyiro.” Jimbo la Bariadi lina wagombea 12 ambao ni Godwin Simba, Mshuda, Masanja Madoshi, Seni Silanga, Manyangu Kulemwa, Zacharia Shigukulu, Maendeleo Makoye, Sweya Makungu, Sitta Mulomo, Wilson Limbu, Slivatus Masanja na Ntemi Ndamo.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Mapenzi Yamtokea PUANI Davina
Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya amedaiwa kutoswa na mwanaume aliyemuachanisha na mumewe ambaye alikuwa bosi wake kwenye kampuni moja iliyopo Kinondoni jijini Dar. Chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, baada ya Davina kuzinguana na mumewe kisa kikiwa ni bosi huyo (Jina tunalihifadhi kwa sasa) alifunguliwa ofisi maeneo ya Kinondoni jijini Dar kisha maisha yakaendelea. “Si unakumbuka kuna yule mwanaume ambaye ndiye alimzuzua Davina hadi akaachana na mumewe? Basi baada ya pale Davina alifungiliwa ofisi yeye na Mike (Sangu) iliyokuwa inajihusisha na mambo ya TV ya mtandaoni, mambo yakawa bambam, akasahau hata machungu ya ndoa yake kuvunjika. “Lakini sasa hivi mambo yameharibika, yule kibosile katibuana na Davina, kaamua kuchukua kila kitu katika ofisi ile na kuiacha tupu. Mike ambaye ndiye aliyemshawishi Davina waanzishe hiyo ofisi sasa hivi yuko zake mkoani anampigia debe mgombea wake,” kilidai chanzo hicho na kuongeza: “Sasa hivi Davina anahaha, anajuta kuachana na mumewe.” Davina alipovutiwa waya na kuulizwa juu ya madai ya kutoswa na mwanaume aliyevunja ndoa yake alisema amechoshwa na maneno ya watu kwani hajawahi kuwa na uhusiano na bosi wake huyo. “Mh! Watu wananitungia habari jamani mimi sipendi kwa sababu hawajui tu wanavyoniharibia, sijawahi kuwa na uhusiano na bosi wangu, kuhusu kazi mbona bado naendelea na hivi ninavyokwambia naelekea hapo kazini,” alisema Davina. Akizungumzia ishu hiyo, Mike Sangu aliyekuwa akifanya kazi ofisi moja na Davina alisema: “Hayo mambo ya Davina kuwa na uhusiano na mkurugenzi wetu siyajui, ninachojua kwa sasa tumesimama kidogo kwa sababu tunafanya usaili wa watu ili tufungue televisheni kwa ujumla kwani mwanzo ilikuwa TV Online na hata huyo Davina tumemuambia alete CV,” alisema Mike.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Nikiridhishwa KITANDANI sharti nimsifie mume Wangu- Joyce Kiria
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live, Joyce Kiria ametoa kali ya mwaka kwa kueleza kuwa, akishibishwa vilivyo na mume wake ‘chakula cha usiku’, haoni sababu ya kumsifia kupitia mitandao. Joyce ambaye amekuwa na kusumba na kumpa sifa kemkemu mume wake kila atokapo kula ‘chakula’ hicho ameeleza kuwa, haoni tatizo kufanya hivyo kwa kuwa kila mtu anajua ukiolewa lazima upewe ‘chakula cha usiku’ na ushibe ndipo utaifurahia ndoa. “Mi sioni ajabu jamani kwa sababu ni vitu vya kawaida kabisa, nani asiyejua tumetoka kwa wazazi wetu kwa ajili ya kufuata ‘chakula cha usiku?’ Kwa hiyo sioni hatari kwa kweli, nitaendelea kumsifia mume wangu atakaponipa furaha, ” alisema Joyce.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Belle 9 haamini kama collabo zinaweza kumtoa kimataifa
Belle 9 amedai kuwa kwenye muziki wake haamini kama collabo ni njia sahihi ya kumfikisha kimataifa zaidi. Akizungumza na mtandao huu, Belle amesema wapo wasanii kadhaa walioweza kutoboa bila hata kufanya collabo na wasanii wa mataifa ya nje. “Mimi nimefanya collabo na Joh Makini, I am proud kwa sababu ni msanii mkubwa ambaye anafanya vizuri ndani na nje. Joh is too expensive sio simple tu kufanya naye collabo,” amesema Belle. “Kama unavyojua msanii mkali hawezi kurekodi na msanii mbovu, mimi naamini inawezekana. Mimi naamini collabo sio kitu kinawezeka kunifikisha International, sijui wasanii wenzangu wengine. “Kwa sababu mtu kama Gsan alishiriki mpaka cipher ya BET najua sio kawaida, sasa Gsan alifanya collabo na nani? Na ni washkaji ambao walikuwa level kubwa. “Mimi siamini collabo inaweza kunifikisha huko, yaani siamini katika collabo kwa sababu ningekuwa nimeshafanya na nimesharelease. “Lakini najua collabo ni maisha ya muziki ambayo inatokea ukafanya lakini mimi sijafikiria nijaribu kufanya ndio nifike huko,” aliongeza muimbaji huyo. Belle anajiandaa kuachia video ya wimbo wake ‘Shauri Zao’ iliyoongozwa na Hanscana.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Batuli kufuata nyayo za Kanumba, ajipanga kuandaa filamu yenye bajeti kubwa
Msanii wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amesema mashabiki wake wa filamu wasione yupo kimya kwakuwa yupo kwenye mpango kuthubutu kama alivyothubutu marehemu Steven Kanumba kwa kuaanda filamu itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 40. Batuli ameuambia mtandao huu kuwa licha ya kuwa anafanya filamu zilizozoeleka, anajipanga kufanya kitu kikubwa ili kuipa heshima tasnia ya filamu nchini Tanzania. “Kazi zangu zinaenda bomba lakini kuna kazi ambazo zinahitaji udhamin Kwa sababu ni kazi tofauti na hizi zilizozoeleka.Inahitaji watu wengi, kazi inayohitaji milioni 40 na kuendelea. Kwahiyo tunahitaji udhamini kwa sababu ni tofauti na filamu hizo ambazo tumezizoea,” amesema muigizaji huyo. “Ni filamu ambayo ipo kijamii zaidi, imezama ndani zaidi, yaAni nafanya kitu kikubwa bila kujua nitapata nini. Nataka kuthubutu kama alivyothubutu Kanumba na ndo maana nipo cool nahangaikia udhamini ili nikamilishe hili. “Mpaka sasa hivi huu ni mwezi wa 5 nipo kwenye maandalizi na bado naona itafika mpaka mwezi wa 12, kwahiyo wadau wasubirie. Ila pia kuna kazi filamu hizi za kawaida zitaendelea kutoka,” ameongeza Batuli. Katika hatua ngingine Batuli amewapongeza wasanii waliojitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali za siasa huku yeye akitoa sababu ya kukaa pembeni kwa wakati huu. “Mimi nitatangaza nia yangu wakati ukishafika, inawezekana labda kuna kitu nakitaka labda sio uwaziri labda ni kitu fulani ambacho kinafanana na kitu kama hicho. “Pia nawapongeza wote waliotangaza nia, wameonyesha kujiamini. “Pia naomba wawapokee wasanii wenzangu sio wote ila wale ambao wanawaona wanafaa kwa sababu sio wote wanafaa hata kwenye watu kumi kuna wa kwanza mpaka wa kumi. Kwahiyo wawapokee wasanii wenzangu kwenye siasa.”
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Rais Kikwete apewa Tuzo ya Utawala Bora
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ametunikiwa Tuzo ya Utawala Bora Afrika kwa mwaka 2015 kutokana na jitihada zake za kudumisha na kuimarisha utawala bora nchini. Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ilieleza kuwa Rais Kikwete ametunikiwa tuzo hiyo na Taasisi ya African Archievers Awards yenye makao makuu nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete anaungana na Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini aliyekuwa wa kwanza kupewa tuzo hiyo mwaka 2011 kutokana na mchango wake wa kutetea haki za binadamu, usawa na amani. “Rais Kikwete ameteuliwa kutoka miongoni mwa watu 1,202 ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye jopo la kimataifa, linalojitegemea na lenye wajumbe kutoka Uingereza na Afrika Kusini kwa ajili ya uteuzi,” ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo iliongeza kuwa, kutokana na tuzo hiyo, Rais Kikwete amealikwa kwenda kuipokea nchini Afrika Kusini kesho mjini Johannesburg. Hata hivyo, Rais Kikwete hataweza kwenda kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi, hivyo badala yake atakwenda Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro. Katika barua ya kumjulisha Rais Kikwete kuhusu uteuzi wake, Mtendaji wa African Achievers Awards, Rex Indaminabo alisema: “Uongozi wa African Achievers Awards unayo furaha kukujulisha juu ya uteuzi wako wa kupokea Tuzo katika kundi la Utawala Bora Afrika.” Mtendaji huyo aliongeza: “Ni kwa furaha na heshima kubwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri na Taasisi ya Uongozi na Menejimenti wanakupongeza kwa mafanikio haya.”
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Cristiano Ronaldo ni kila kona yeye na mtoto wake, mama yake atafahamika? Haya hapa mengine kama yalikupita..
Cristiano Ronaldo ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania , mara nyingi akiwa anakula good times zake utaona jamaa yuko na mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior na huwa anamuwekea ulinzi wa kutosha kila anapokatisha. Cristiano Ronaldo Junior alizaliwa June 17 2010 San Diego Marekani wakati ambao Ronaldo alikuwa Afrika ya Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia, Ronaldo alitangaza 3 July 2010 kuhusu kupata mtoto kupitia account yake ya Twitter na Facebook siku chache baada ya Ureno kutolewa na Hispania katika michuano ya Kombe la Dunia. Baada ya Ronaldo kutangaza taarifa hizo za kuwa baba wengi wamekuwa wakijiuliza na kutaka kumjua mama wa mtoto huyo licha ya Ronaldo kutotaka kumuweka wazi baada ya maelezo aliyoandika katika account zake Mitandaoni kwamba hiyo kitu inahusu maisha yake binafsi na haitaji kuweka wazi. “Nikiwa na furaha tele na hisia za kuwataarifu kwamba hivi karibuni nimekuwa baba wa mtoto wa kiume. Kama nilivyokubaliana na mama wa mtoto kuwa jambo hili kuwa siri. Mwanangu atakuwa chini ya uangalizi wangu. Naomba kila mtu aheshimu haki ya kuwa na usiri angalau kwa masuala binafsi kama haya”> > > Ronaldo Licha ya kuwa mama wa mtoto hajulikani ila kumekuwa kuna taarifa za kichunguzi amabazo zinasema miezi kadhaa baada ya Cristiano Ronaldo Jr kuzaliwa mama yake alifariki lakini taarifa nyingine zinasema Cristiano Ronaldo Jr alizaliwa na kwa njia za kitechnolojia ( Surrogate Mother ) ambapo mwanamke wa kimarekani alilipwa na Ronaldo pound milioni 10 ambayo sawa na bilioni 32 za kitanzania ili abebe ujauzito kiteknolojia zaidi. Ronaldo akimpeleka mwanae shule Baada ya malipo kufanyika Ronaldo na mama wa mtoto wake wamekubaliana kisheria kuwa asije akajitokeza hadharani na kusema yeye ni mama wa mtoto wa Ronaldo . Ronaldo kwenye tuzo za Ballon D’OR 2013 pembeni ni mpenzi wake wa zamani Irina Shayk Ronaldo aliposhinda goli wakati mwanaye akiwepo uwanjani na kushangilia kwa kunyonya kidole kama mtoto
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Video ya Rais Obama alivyosalimia kwa Kiswahili Kenya
Ndege ya Rais Obama ilitua July 24 2015 saa mbili usiku Jomo Kenyatta International Airport , Historia ikaandikwa kwa Rais huyo wa kwanza wa Marekani kutembelea Kenya. Obama ni mmoja ya Marais wacheshi sana na wanaopenda stori za utani utani hivi wakati mwingine. July 25 2015 Rais Obama amefungua Kikao cha Global Entrepreneurship Summit Nairobi Kenya, baada ya kukaribishwa na mwenyeji wake, akasalimia kwa kiswahili cha Wakenya kabisa; “Niaje wasee……. Hawayuni ” Hiki hapa kipande cha Video wakati Rais Obama anasalimia kwa kiswahili.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Video fupi ikimuonyesha Rais Obama akicheza wimbo wa Sauti Sol Kenya.
Sauti Sol ni kundi maarufu la muziki kutokea nchini Kenya ambalo limefanikiwa kuvuka hata mipaka na kuteka kwenye nchi jirani kama Tanzania, Rwanda, Burundi na nchi nyingine za Afrika mpaka kupelekea kuwa nominated kwenye tuzo kubwa kama za MTV na BET 2015. Kundi hili lilipata mwaliko maalum wa kwenda kuimba Ikulu ya Kenya kwenye party ya kumkaribisha Rais Barack Obama wa Marekani ambaye baba yake mzazi ni mzaliwa wa Kenya. Tazama kwenye hii video fupi hapa chini jinsi Sauti Sol walivyokuwa wakiperfom na baadae Rais Obama na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuungana nao kucheza.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Obama Aitaka Kenya iongeze Mapambano dhidi ya al Shabaab
Rais wa Marekani Barack Obama jana (25.07.2015) alifanya mashauri na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi na kujadili maswala kadhaa yakiwemo usalama, uwekezaji na uongozi. Rais wa Marekani Barack Obama ameitaka Kenya kuongeza jitihada za kulikabili kundi la wanamgambo wa al Shabaab kutoka Somalia. Obama amesema Marekani inahitaji kushirikiana kwa karibu zaidi na Kenya kuliangamiza kabisa kundi hilo, ikiwa ni pamoja na kubadilishana taarifa za kijasusi. Kiongozi huyo amesema mitandao ya kundi la al Shabaab imedhoofishwa katika Afrika Mashariki lakini kitisho bado kingalipo. “Tumelipunguza eneo linalodhibitiwa na Al-Shabaab. Tumefaulu kupunguza udhibiti wao nchini Somalia na kuidhoofisha mitandao yao hapa Afrika Mashariki. Hiyo haina maana tatizo limetatuliwa,” alisema Obama wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta. “Tunaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa uwezo wa makundi ya kigaidi, lakini bado yanaweza kusababisha maafa,” akaongeza kusema Obama. Rais Obama aliandaliwa gwaride la heshima katika Ikulu ya Rais kabla ya kufanya mashauri na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta. “Tumekuwa na mazungumzo ya kufanya na Rais Barack Obama juu ya maswala muhimu yanayohusu Kenya na Marekani kama vile usalama na uhusiano wa kimaendeleo miongoni mwa maswala mengine,” alisema Uhuru. Mikataba yasainiwa Mikataba kadhaa ya ushirikiano imetiwa saini ukiwamo ule wa ushirikiano katika swala la ugaidi. Rais Obama alisema, “Leo( jana ) tumezungumzia suala la kuimarisha uhusiano wetu wa kiusalama kama sehemu yetu ya maongozi pia tumezungumzia mikakati ya kukabiliana na itikadi kali hapa nchini na dunia nzima kwa ujumla.” Marais hao wawili jana asubuhi walifungua kongamano la sita la ulimwengu kuhusu ujasiriamali katika ofisi za kabla Rais Obama kuzuru eneo la shambulizi la bomu la Agosti 7 mwaka 1998 na kuweka shada la maua kama ishara ya kuwakumbuka wahanga wa shambulizi hilo lililotekelezwa katika ubalozi wa Marekani wakati huo. Kwenye kongamano hilo la ujasiriamali Rais Kenyatta alisema, “Nchi hii na bara hili hatuwezi kusema hatufanyi makosa lakini bila shaka tunaweza kudai kwamba tunasonga mbele. Cha msingi nikwamba tuko katika safari tunayowaalika mjiunge nasi. Tunaona nafasi nzuri inahitaji kuheshimu haki za binadamu.” Kongamano hilo la ujasiriamali linahudhuriwa na wajumbe wapatao 4,000 kutoka mataifa 120 ulimwenguni. “Changamoto ni nyingi. Ni vigumu kupata mikopo, ni vigumu kupata mafunzo na ujuzi wa kuendesha biashara na zaidi ya yote ni vigumu kwa wanawake na vijana ambao hawapati nafasi za juu za uwekezaji.” Viongozi hao wawili wamewahimiza vijana kuzingatia ufumbuzi unaolenga kutatua matatizo ya bara la Afrika. Kutokana na makubaliano hayo ya kibiashara, mipango inafanywa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi Marekani. Ziara ya Rais Barrack Obama nchini Kenya haikuwa tu ziara ya kikazi bali pia kukutana na familia yake kwani alipata fursa ya kujiunga na jamaa zake kutoka kijiji cha Kogelo kaunti ya Siaya kwa chakula cha jioni katika hoteli moja ya kifahari alipowasili jijini Nairobi hapo juzi. Leo Rais Obama anatarajiwa kutoa hotuba ya hadhara katika uwanja wa michezo wa kimataifa wa Kasarani na kisha kuondoka nchini kwenda Addis Ababa Ethiopia kwa kongamano la viongozi wa Umoja wa Afrika.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Batuli: Rushwa ya Ngono iliniondoa Kaole
Msanii wa bongo movie Batuli ameweka wazi kuwa alikimbia kundi la Kaole sanaa Group baada ya kukutana na changamoto nyingi ikiwepo changamoto ya rushwa ya ngono. Batuli alifunguka hayo Jumatano alipokuwa katika kipengele cha Kikaangoni kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV. Batuli alifunguka na kusema kuwa moja ya sababu kubwa ambayo ilimfanya kuondoka katika kundi hilo ilikuwa kuombwa rushwa ya ngono ili aweze kupewa kipaumbele zaidi kuliko wasanii wengine jambo ambalo kwa upande wake hakuwa tayari kulifanya na kuamua kuondoka katika kundi hilo. Batuli anasema kabla ya kuweza kutoka kupitia mkono wa Kanumba alishasota sana katika kundi hilo na alikuwa akibaniwa nafasi kutokana na kutokubaliana na watu ambao walikuwa wakimtaka kingono ili waweze kumpa kipaumbele zaidi, ndipo hapo alipoamua kuondoka na baadaye msanii Kanumba ndipo alipoamua kumpa nafasi na kuweza kumtoa kisanaa. “Nilijiunga kaole lakini baadae Kanumba aliniona nafaa kwenye filamu chini ya kampuni ya Game 1st Quality ndivyo nilivyotoka ila kabla ya hapo nilisota sana kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwepo kubaniwa kazi, na kutakwa kimapenzi au kuombwa rushwa ya ngono. “Moja ya jambo lililofanya niondoke Kaole ni changamoto ya rushwa ya ngono, nilikutana na changamoto hiyo nilipojiunga na kikundi cha kaole nikaamua kuhama kikundi kabisaa” “Nilijiengua kaole baadae Kanumba alinishika mkono” Aliongeza Batuli Mbali na hilo Batuli alisema kuwa kwa sasa yeye ni mtalaka na ana watoto wawili na katika kipindi chake cha ndoa hakuwahi kuchepuka hata siku moja sababu huwa anapenda kutulia na mtu mmoja, na kuweka wazi kuwa katika maisha yake hajawahi kugombanisha wanaume sababu huwa anapenda kuwa na mtu mmoja anayempenda. “Hapana haijawahi kutokea nimegombanisha wanaume au wanaume wamegombana kwa sababu yangu kwa kuwa huwa sina mahusiano mengi natulia na mmoja” Tunatambua katika tasnia ya filamu na movie nchini wasanii wengi wamekuwa wakitumia kiki na skendo mbalimbali kama njia ya kujitangaza na kujiongezea umaarufu zaidi katika sanaa husika jambo ambalo kwa Batuli limekuwa kinyume chake. Yeye anaamini kuwa skendo na kiki zinamfanya msanii adharaulike na kushusha heshima ya msanii huyo jambo ambalo yeye ameweza lifananisha na vazi baya au chafu katika tasnia ya filamu na sanaa kiujumla. “Sio kweli, huwezi kuheshimika na scandals kuna mfanya msanii adharaulike kila aendapo. Naweza kusema scandals ni vazi baya na chafu kwenye tasnia yetu”
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Diamond Platnumz ashinda tuzo nyingine Afrika Kusini ‘African Achievers Awards’.
Rais Kikwete Ateua Mkurugenzi mpya wa Tume ya Uchaguzi
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa kumteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Tume hiyo, Kailima Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi. Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Kombwey ambaye aliapishwa jana jioni, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba, ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Rais Kikwete pia amemteua Jaji Richard Mziray, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na majaji wengine wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Taarifa hiyo pia imesema kuwa Jaji Mziray ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam. Majaji wengine wa Mahakama Kuu walioteuliwa na Rais Kikwete ni Ignas Kitusi ambaye ni Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania na Wilfred Dyansobera, ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu. Wengine ni Lameck Mlacha ambaye ni Naibu Msajili na Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi; Salima Chikoyo ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi; Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania na Mallaba. Pia yumo Adam Mambi ambaye ni Katibu Msaidizi Tume ya Kurekebisha Sheria; Sirilius Matupa ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Rais, Sheria, Ofisi ya Rais, Ikulu; Issa Maige ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na Licia Kairo ambaye ni Wakili wa Kujitegemea. Dk Masoud Shaaban Benhaji, Wakili wa Kujitegemea na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam pia ameteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu. Wengine ni Victoria Makani ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na Rehema Kerefu ambaye ni Mwanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Magufuli Awataka Wananchi Wachague Wabunge Wachapakazi wa CCM Ili Iwe Rahisi Kwake Kuunda Baraza Zuri la Mawaziri
MGOMBEA urais mteule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amewaomba wananchi wa mkoa wa Morogoro na mingine nchini, kuchagua wabunge wachapakazi kama yeye wanaotokana na CCM. Lengo la ombi hilo, ni ili yeye atakapochaguliwa na Watanzania kuwa Rais, ateue wabunge hao kwenye nafasi ya uwaziri watakaowatumikia kikamilifu. Akielezea uzoefu wake, Dk Magufuli alisema ametumikia nafasi ya ubunge na uwaziri katika miaka 20 na anajivunia kuwa na rekodi nzuri ya utendaji, hivyo alisema anatumia fursa hiyo, kuwaomba wananchi wa mkoa wa Morogoro, wachague wabunge wanaofanana naye wanaotokana na CCM. Dk Magufuli alisema hayo juzi kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Dumila na Dakawa wilayani Mvomero na Manispaa ya Morogoro katika viwanja vya Jengo la CCM Mkoa, wakati akisalimia na kujitambulisha kwa wananchi, wapenzi na wanachama wa CCM. “Wananchi wa Morogoro nawaombeni muwachague wabunge wachapakazi wanaotokana na CCM kama nilivyokuwa mimi, ili nitakapopata ridhaa yenu ya kuchaguliwa kuwa Rais wenu, niwateue kuwa mawaziri ili wawatumikie kikamilifu hasa wananchi wa hali ya chini,” alisema mgombea huyo. Alisema iwapo Watanzania watampa ridhaa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, atahakikisha anamaliza migogoro baina ya wafugaji na uwakulima hapa nchini. Magufuli alipokewa na umati mkubwa wa wananchi katika maeneo ya Dumila na Dakawa huku wakimshangilia na kumpongeza wakimuita ‘jembe’, ambapo wakati akizungumza nao, alisema anasononeshwa na kero ya kuwepo kwa migogoro ya wakulima na wafugaji. Aliahidi kuwa akipewa ridhaa ya kuwa Rais atakomesha jambo hilo. Alisema, migogoro hiyo imekuwa ikigharimu maisha ya watu na haipaswi kuendelea kuwepo hapa nchini, kwakuwa Watanzania wote wamekuwa wakiishi kama ndugu bila kujali dini wala kabila, hivyo ni lazima ikomeshwe ili amani iendelee kuwepo katika maeneo yote. Magufuli alisema, kinachotakiwa kufanyika ni kukutanisha pande zote mbili za wafugaji na wakulima na kuzungumza pamoja ili kupatikana muafaka pasipo kuangalia itikadi ya vyama vya siasa, kabila wala rangi. Awali, Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Morogoro, Kanali mstaafu Isaac Mwisongo ambaye wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais kupitia chama hicho alitangaza hadharani yeye na wazee wenzake, kumuunga mkono Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, alisema kuanzia sasa wanaungana na Dk Magufuli. Alisema yeye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Morogoro, Stephen Mashishanga, na Waziri wa zamani aliyeshika nyadhifa mbalimbali katika serikali za awamu ya tatu na nne, Dk Juma Ngasongwa walipanda jukwaani na kumuunga mkono Lowassa, lakini kutokana na kumalizika kwa mchakato huo, sasa wameunganisha nguvu zao zote kwa Dk Magufuli, ambaye ni mgombea urais wa CCM.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Nyambari Nyangwine Awalalamikia Vijana wa CCM Kumzomea Hadharani
MBUNGE wa Jimbo la Tarime anayemaliza muda wake, Nyambari Nyangwine, amedai kuchezewa rafu akisema kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakinywa pombe aina ya viroba kwa ajili ya kumzomea ili aonekane hakubaliki kutetea nafasi yake. Nyangwine ambaye anatetea nafasi yake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa akigombea Tarime Vijijini, ametaka mchatako wa kumpata mgombea ambaye atapeperusha bendera ya CCM kuwania ubunge katika jimbo kufanyika kwa ustaarabu. Alisema amelikemea jambo hilo katika vikao vya ndani huku akiwaomba wagombea wenzake kuheshiminiana na kuongeza kuwa angependa uchaguzi uwe huru na haki na kuwataka wagombea wenzake wasilazimishe kukubalika. Hata hivyo, Nyangwine alisema ahadi alizitoa kwa wananchi wa Tarime katika uchaguzi wa mwaka 2010 zimetekelezwa kwa asilimia zaidi ya 90 na kwamba ana imani atashinda tena kwani wananchi wa Tarime wanaona kazi kubwa ambayo ameifanya katika kipidi chake cha miaka mitano. Nyangwine alisema endapo atateuliwa tena kuwania ubunge atahakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Jimbo la Tarime Vijijini.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Picha ya Diamond na Zari Wakiwa Nusu UCHI Yawavuruga Mashabiki…
Stori zilizo zagaa mtaani ni kuwa wawili hawa( Diamond na Zari ) wanatarajia kupata mtoto wao hivi karibuni, lakini picha hii imeibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki wa mastaa hawa. Kundi kubwa kubwa linawalaumu wasanii hawa kwa kupiga picha kama hii huku likidai ni kumdhalilisha mtoto aliyeko tumboni. Aunt Ezekiel aliwahi piga picha kama hii nakujikuta akioga mvua ya matusi toka kwa mashabiki wake.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Zitto Kabwe: Hatuna Mpango wa Kujiunga na UKAWA
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema hakipo tayari kujiunga na Ukawa kama ambavyo habari za uvumi zimekuwa zikizagaa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa chama hicho kipo mbioni kujiunga na Ukawa. Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe jana na kusema kuwa taarifa zinazoenea kuwa chama hicho kitajiunga na Ukawa sio za kweli. “Leo( jana ) siku nzima nilikua nina kikao cha mashauriano na viongozi wa chama wa kata zote za mkoa wa Dar es salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya Dar) jumla ya wajumbe 1023 walihudhuria, tumesisitiza kuwa hatutajiunga UKAWA… “Ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya chama ndani ya UKAWA kilitangaza kuwa hawatutaki. “Hata juzi kwenye gazeti la Mawio waliandika kuwa tumefukuzwa UKAWA, sisi tumeamua kuingia kwenye uchaguzi wenyewe.. “Tarehe 10 Agosti 2015 tutatangaza mgombea Urais tutakayemuunga mkono baada ya mkutano mkuu wa kidemokrasia wa ACT Wazalendo. “Tutanadi #AzimioLaTabora kama zana ya kuleta mapinduzi katika nchi yetu,” alisema Zitto Kabwe Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa chama cha ACT Wazalendo kipo katika mchakato wa kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ili kuongeza nguvu umoja huo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat
Mbowe Aundiwa Zengwe Ubunge Hai
Wanachama wa Chadema wamedai kufichua mpango unaofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM wa kumwekea pingamizi Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe ili asiwanie ubunge. Kiini cha mipango hiyo ni hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Hai iliyomtia hatiani kwa kosa la kumshambulia mwangalizi wa ndani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Nassir Yamin. Katika hukumu hiyo, iliyotolewa Juni 17 na Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Hai, Dennis Mpelembwa alimhukumu Mbowe kulipa faini ya Sh1 milioni au kwenda jela mwaka mmoja. Hata hivyo, Mbowe ambaye ni mgombea pekee na kushinda kura za maoni kwa kupata 269 za ndiyo na tano za hapana, alilipa faini hiyo na kuachiwa huru baada ya wafuasi wake kuchanga fedha hizo. Mipango hiyo inayodaiwa kuwa ni ya CCM kutaka kutumia hukumu hiyo kumzuia Mbowe kuwania ubunge, ilielezwa juzi katika Mkutano Mkuu maalumu wa kura za maoni za ubunge Jimbo la Hai. Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, James Swai alimuuliza Mbowe amejiandaaje, kwa sababu kuna madai kuwa CCM wana mpango wa kutumia kesi hiyo ili kumwengua kugombea nafasi hiyo. Hata hivyo, wakati akijibu swali hilo, Mbowe hakueleza wazi kama anafahamu mpango huo zaidi ya kuitaka CCM isitafute ushindi wa mezani. “Wangekuwa na wanasheria wasingefikiria kabisa wala kuzungumza hivyo. Kifungu nilichohukumiwa nacho hakinizuii kugombea. Wasitafute ushindi wa mezani waje uwanjani,” alisema Mbowe. Mbowe alisema tayari jopo la mawakili sita wa Chadema, ambao hata hivyo hakuwataja kwa majina, limeweka mkakati maalumu wa kukata rufaa kupinga hukumu hiyo aliyodai ni batili.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat