Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all 2247 articles
Browse latest View live

Wiki Ya Mtikisiko: Lowassa na Timu Yake Wasubiriwa kwa Hamu UKAWA…….Zaidi ya Viongozi 950 Wa CCM Kutimkia CHADEMA Wiki hii

$
0
0

Ni wiki ya mtikisiko. Hivi ndiyo unavyoweza kuelezea hali itakavyokuwa nchini kutokana na matukio makubwa ya kisiasa yanayotazamiwa kutokea ndani ya wiki inayoanza leo ambayo yanaweza kubadili mwelekeo wa siasa za Tanzania. Hali hiyo inatokana na vuguvugu la kisiasa linalohusisha viongozi wenye ushawishi kuhama vyama vyao vya siasa na kutimkia kwenye vyama vingine, ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu. Ni wiki ambayo itapambwa na matokeo ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa CUF kilichofanyika jana mjini Zanzibar kuhusu mustakabali wake ndani ya Ukawa, ikizingatiwa kuwa hivi karibuni chama hicho kiliamua kujiweka kando ya vikao vya umoja huo hadi vikao vya juu viamue. Hata hivyo, habari ambazo tumezipata zinasema kuwa uwezekano wa chama hicho kujitoa ndani ya Ukawa ulikuwa mdogo kutokana na kuogopa hasira za wananchi wenye matumaini na umoja huo. Aidha, kulikuwa na taarifa kuwa kikao cha jana kilikuwa kinaangalia jinsi watakavyoshiriki katika umoja huo na kwamba kulikuwa na matumaini makubwa. Vile vile, hii ni wiki ambayo kura za maoni zinazoendelea katika vyama vikubwa vya siasa, kuonyesha baadhi ya vigogo wakiangushwa na kujaribu kutafuta upenyo wa madaraka katika vyama vingine. Pia, ni wiki ambayo chama kikuu cha upinzani, Chadema kimeamua kusogeza mbele tarehe za kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais kutoka jana hadi Ijumaa, katika kile kinachotazamwa kama kusubiri mchakato wa kumpata mgombea urais. Kana kwamba hiyo haitoshi, hii ni wiki ambayo minong’ono ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye jina lake limekatwa katika orodha ya wasaka urais wa CCM anaweza kuhamia Chadema. Tayari baadhi ya viashiria vya hali hiyo vimeanza kuonekana ambapo wiki iliyopita wabunge wawili wa chama tawala cha CCM, James Lembeli na Ester Bulaya waliachana na chama hicho na kujiunga na Chadema huku chama hicho cha upinzani kikitamba kujiandaa kuwapokea vigogo wengine zaidi. Kiashiria kingine cha mtikisiko ni hatua ya madiwani 18 wa CCM wilayani Monduli na wengine 10 wa UDP na CCM Bariadi kuhamia Chadema. Lakini pia wapo wabunge na madiwani wanaohama Chadema kwenda chama cha ACT-Wazalendo. Vuguvugu hilo la kisiasa limekolezwa na kauli za wanasiasa wawili vijana kwa nyakati tofauti, Godbless Lema na Zitto Kabwe kuwa wiki hii itakuwa ya mshikemshike kutokana na mambo yaliyopangwa kufanyika. Zitto: Ni wiki ya mabadiliko Akiandika kwenye kurasa zake za Facebook na Twitter jana, Zitto alisema, “Wiki ya kuanzia Jumatatu tarehe 27 Julai 2015 itashuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye siasa za Tanzania. Kuimarika kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ni jambo jema kwa nchi yetu.” Alipotakiwa kufafanua kauli yake, Zitto hakutaka kutaja matukio husika, lakini alisisitiza kuwa mtikisiko wa kisiasa utatokea na mazingira ya hali hiyo yataanza kubadilika kuanza kesho. “Na huu ujumbe nilioandika hauna uhusiano na chama cha ACT-Wazalendo,” alisema. Alipotakiwa kufafanua zaidi, alisema “Watanzania wasubiri mabadiliko ya siasa za Tanzania.” Lema asema ni mtikisiko Kwa upande wake Lema, akiwa jimboni kwake Arusha, alisema wiki hii itakuwa ya mtikisiko kwa CCM kwa sababu zaidi ya viongozi wake 950 kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na taifa watahamia Chadema. Akizungumza wakati wa kuwapokea vigogo watatu na wanachama 30 kutoka CCM jana, Lema alisema kuanzia kesho kimbunga cha viongozi na wana CCM kuhamia Chadema kitavuma kila kona ya nchi. Vigogo hao ni Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Matthysen na mwenyekiti wa CCM Kata ya Terat, Simon Mollel wote wa jijini Arusha. Haya yametokea ikiwa ni siku chache baada ya katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Longido, Tostau Mollel kahamia Chadema, huku baadhi ya watiania wa udiwani na ubunge waliokamilisha maandalizi wakikacha kuchukua fomu za chama hicho. Miongoni mwa waliokacha kuchukua fomu bila kutoa sababu ni mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye, mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha, Robinson Meitinyiku, mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, Mathias Manga na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole, wote wakitajwa kuwa kwenye timu ya Lowassa. “Hii iliyoanzia Bariadi, Monduli, Longido na Arusha mjini ni mvua za rasharasha. Masika yataanza wiki ijayo (kuanzia kesho Jumatatu) kwa zaidi ya viongozi 950 wa ngazi mbalimbali watakapohama CCM na kujiunga Chadema,” alisema Lema. Alifananisha Chadema na kanisa au msikiti akisema milango yake iko wazi kuwapokea wanachama wa vyama vingine wanaotaka kutumikia umma kujiunga nacho kwa kutubu makosa yao na kusamehewa kabla ya kuingia kazini Oktoba 25, mwaka huu. Wabunge wanne Chadema watua ACT Wakati upepo ukivuma kutoka CCM kwenda Chadema, hali kama hiyo imekinufaisha chama kipya cha ACT-Wazalendo baada ya kuvuna wabunge watatu wa viti maalumu na diwani mmoja kwa mpigo kutoka Chadema. Wabunge hao ni Mhonga Ruhwanya (Kigoma), Chiku Abwao (Iringa ) na AnnaMaryStella Mallac (Mpanda) wote kutoka Chadema, huku mwingine ambaye jina lake tunalihifadhi kwa kuwa hatukumpata, akitimkia CCM. Wabunge hao wanaungana na Mbunge wa Kasulu mjini, (NCCR – Mageuzi ) Moses Machali aliyehama kutoka NCCR-Mageuzi kwenda ACT Wazalendo, hivi karibuni. Akizungumza na mwandishi jana, Zitto alisema atawatangaza wakati wowote wabunge wengine sita kutoka CCM, Chadema na CUF. Kauli ya Chiku Abwao Akizungumza kwa simu akiwa India, Abwao alikiri kuhamia ACT-Wazalendo akidai kutoridhisha na mwenendo wa Chadema na hasa taarifa anazosikia za Lowassa ambaye amekuwa akituhumiwa mambo mbalimbali kuhusishwa na Chadema. “Mimi kwa historia yangu kitu kilichonipeleka upinzani ni kutafuta haki uwajibikaji na kupinga vitendo vya ufisadi na rushwa, lakini nimekishangaa chama changu katika suala hili,” alisema. “ Licha ya mambo ya sintofahamu yanayoendelea Chadema lakini hili la Lowassa kama kweli atajiunga na chama hiki basi suala litakuwa ni moja tu, ni chaneli ya kuingia Ikulu, lakini haya mambo mimi siyapendi kwa sababu ni mtu wa kupinga ufisadi na kupigania haki za wanyonge,” alisema Abwao Alisema ameamua kuhamia ACT-Wazalendo, kwa sababu ni chama pekee kitakachowakomboa Watanzania na kwamba ataenda moja kwa moja kugombea jimbo la Iringa Mjini badala ya Isimani. “Niliamua kwenda Isimani kipindi kile ili kuijenga Chadema, lakini safari hii nipo huku ACT-Wazalendo nitaenda kupambana na Mchungaji (Peter) Msigwa na yeyote yule atakayepitishwa na CCM,” alisema Abwao. Mhonga: Ni uamuzi tu Mhonga Rhuwanya alipouliwa alijibu kwa kifupi, “Kama ulivyosikia ndiyo hivyo hivyo, mimi ni mtu mzima na nina maamuzi yangu kwani chama siyo dini.” Alipoulizwa atagombea ubunge kupitia ACT-Wazalendo, alijibu, “Kwani mtu akihamia chama kingine ni lazima agombea ubunge… hata hivyo naweza kugombea tena.” Mallac aenda kupokewa Kwa upande wake, Mallac alisema alikuwa safarini kwenda Katavi kupokewa ACT-Wazalendo. “Niko njiani naelekea Katavi mkoani kwangu kupokewa rasmi na kiongozi wangu wa chama cha ACT –Wazalendo, Zitto Kabwe,” uliosomeka ujumbe mfupi wa maneno. Zitto awapokea Zitto alisema huo ni mwendelezo wa chama hicho kuwapokea wabunge kutoka katika vyama mbalimbali na hivi karibuni atawapokea wengine katika mikoa ya Kagera, Tabora, Rukwa na Zanzibar. “Tabora wako wawili na Kagera mbunge mmoja wote wa CCM, kutoka wilaya ya Karagwe, pia Zanzibar wawili kutoka CUF na Chadema. Hawa wote wanasubiri mchakato wa kura za maoni umalizike ndipo tuwatangaze. “Hawa wabunge tuliowapokea ni sawa na asilimia 10 kati ya 50 niliosema, maana watu walikuwa wananiuliza, ‘Zitto ulisema utawapokea wa kiasi kadhaa mbona kimyaa?’ mambo ndiyo yameanza sasa.” Diwani Chadema atua ACT Katika hatua nyingine, aliyekuwa diwani wa Kata ya Segerea (Chadema), Azuri Mwambagi amejiunga na ACT-Wazalendo kwa sababu ya uhusiano mbaya kati yake na viongozi wa Chadema wa jimbo hilo. Mwambagi alisema kuwa amekuwa diwani wa kata hiyo kwa miaka mitano lakini hakukuwa na ushirikiano mzuri kati yake na uongozi wa jimbo hilo. “Kila ninachokifanya wenzangu wanasema sijafanya kitu na wanaamua kunizunguka kwa wananchi, hali hii imenichosha,” alisema Mwambagi. Katibu wa jimbo hilo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Anna alisema hata yeye amezisikia taarifa za diwani huyo kuhamia ACT- Wazalendo, lakini akakana kuwapo mizengwe aliyofanyiwa Mwambagi. “Tupo katika mchakato wa kura za maoni na yeye ameomba kuteuliwa kugombea udiwani Kata mpya ya Liwiti, kama anahisi alikuwa kiongozi bora enzi za utawala wake kwa nini asisubiri matokeo ya kura za maoni ndipo afanye uamuzi huo?” alihoji Anna. (Imeandikwa na Bakari Kiango na Peter Saramba-Mwananchi)

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


KTM Issues Recall For 1290 Super Duke R

Casey Stoner’s Crash At Suzuka 8 Hours Is Quite Terrifying [Video]

Lowassa Akaribishwa Rasmi UKAWA……Hapa kuna picha na kilichojiri Leo Katika mkutano wa UKAWA na Waandishi wa habari

$
0
0

“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje”. Hii ni moja ya kauli ambayo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM. CCM ilikuwa na Wagombea zaidi ya 40 ambao walitangaza nia na kuchukua fomu za Kugombea Urais 2015 lakini baadae Chama hicho kikampitisha Dk. John Pombe Magufuli kugombea nafasi hiyo, baada ya hapo kukawa na taarifa nyingi sana kuhusu ishu ya Edward Lowassa na UKAWA. Viongozi wa Umoja wa UKAWA wamekutana Dar leo na mmoja wa Viongozi hao, James Mbatia amesema wamekubaliana kumkaribisha Mbunge Edward Lowassa ndani ya UKAWA na wako tayari kumpa nafasi na kushirikiana nae. Mbatia ameongeza kuwa Lowassa ni mchapa kazi makini na mfuatiliaji wa karibu wa kiutendaji katika majukumu anayokabidhiwa. Alipoulizwa kuwa Lowassa atakuwa mgombea Urais Mbatia amesema kila chama kina utaratibu wake hivyo mchakato ukishakamilika atatangazwa mgombea urais wa UKAWA mmoja mwanzoni mwa mwezi agosti.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Tatizo la mashine kutotambua alama za vidole limejitokeza katika baadhi ya vituo jijini DSM.

$
0
0

Tatizo la mashine kutokutambua alama za vidole limejitokeza kwa baadhi ya vituo wakati zoezi la uandikishaji likiendelea jijini Dar es Salaam na kusababisha mashine kuzima zaidi ya mara sita huku tatizo la ubovu wa mashine na waandikishaji wasiokuwa na uzoefu likiendelea kulalamikiwa. Licha ya kuwepo kwa malalamiko tangu siku ya kwanza ya zoezi hili kuanza hapa jijini lakini mamlaka husika zimeonekana kushindwa kuyatatua kwa wakati hali inayopelekea msongamano kwa baadhi ya vituo kutokupungua na watu kulazimika kuamka usiku wa manane kuwahi namba za uandikishwaji siku moja kabla.   ITV imetembelea vituo mbalimbali na kushuhudia wananchi wakiwa wamejipumzisha vivulini na wengine wakichapa usingizi wakisubiri kuitwa majina huku kina mama wenye watoto wakilalamikia kutokupewa kipaumbele.   Baadhi ya waandikishaji waliozungumza na ITV wamedai kuwa tatizo la vidole vya baadhi ya wananchi kutokusoma kwenye mashine limekuwa likijitokeza mara kwa mara na kulazimika kutumia muda mwingi kuhudumia mtu mmoja hali inayozua kelele kwa watu waliopo kwenye foleni.   Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke akizungumzia zoezi hilo amesema changamoto ambayo wamekuwa wakikabiliana nayo mara kwa mara ni watu kupiga simu vituoni hasa wanapoona wenzao hawafuati utaratibu na kuongeza kuwa hakuna aliyeshikiliwa kutokana na vurugu zinazojitokeza katika vituo hivyo.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mbunge wa viti maalumu Chadema Chiku Abwao ajiunga na chama cha ACT wazalendo.

$
0
0

Wakati vuguvugu la uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani likiendelea kwa kasi mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha demokrasi na mendeleo chadema Bi.Chiku Abwao amejitoa katika chama hicho na kujiunga rasmi na  chama cha ACT wazalendo. Bi.Abwao amesema ameridhishwa na uongozi wa ACT-wazalendo, katiba na ilani ya uchaguzi wa chama hicho hadi kumpelekea kuamua kujiunga kwa vile kinalenga kumkomboa mtanzania masikini pamoja na kuweka msingi imara ya maadili ya viongozi. Awali akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu wa ACT-wazalendo, katibu wa mipango na mikakati  Bwana Mchanga Habibu amesema chama cha ACT-wazalendo kimepata maendeleo makubwa kwa muda mfupi kutokana na kuwa katiba bora, kufuata azimio la Tabora na ilani ya uchaguzi iliyobora hali inayochangia wanasiasa wengi kujiunga na ACT kwa kuwa ndio chama kinacholenga kuwakomboa wananchi.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Ajali ya Treni yaua wa Nne Tabora.

$
0
0

Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa baada ya Treini ya mizigo,kuligonga basi kampuni ya Don’t Worry lililokuwa likitokea mjiniTabora kuelekea ufuruma  uyui mkoani humo  lilipofika eneo la kuvuko cha reli eneo loa malolo manispaa ya Tabora katika kile kilichodaiwa kuwa ni uzembe wa dereva. Mashuhuda wa ajali hiyo  wamesema kuwa, dereva aliyekuwa katika mwendo wa kasi alitaka kukatiza haraka bila kuzingatia eneo hilo inapopita Treini hata kama aliiona Treini hiyo, na ndipo alipokata kona ya ghafla na basi hilo kuanguka kwenye reli na Treini kuigonga na kukutoa paa lote la juu la gari.   Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora  kamishina msaidizi Juma Bwire amesema kuwa katika ajali hiyo ya basi lenye namba za usajili T568 ABP,wanaume watatu na mwanamke mmoja wamepoteza maisha huku dereva aliyejulikana kwa jina la Kaonjo Iddy (34) akitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo majeruhu wamepelekwa katika hospitali ya rufaa na mkoa wa Tabora.   Viongozi wa shirika la reli waliofika  katika eneo la ajali hiyo wamesema kuwa madereva hawazingatii usalama wa barabarani kwani shirika la reli limejitahidi kuhakikisha linaweka alama husika lakini kutokana na mazoea mabaya hawajali na matokeo ni kusababisha ajali mbaya kama hiyo.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Wayne Rainey To Be Honoured At The AMA Ceremony


Hii ni hukumu iliyotolewa leo JULAI 28 na mahakama ya Libya kwa mtoto wa Gaddafi …

$
0
0

Mahakama ya  Libya leo imetoa hukumu kwa mtoto wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Gaddafi,  aitwaye  Saif al Islam  na wenzake nane kufuatia uhalifu wa kivita uliohusishwa na mapinduzi ya mwaka 2011. Wote walikuwa wameshtakiwa pamoja sasa wamehukumiwa kunyongwa pamoja na washirika wengine wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani kwa kujaribu kazima maandamano wakati wa mapinduzi hayo. Mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi aliyehukumiwa kunyongwa Saif al Islam hakuwepo mahakamani na alitoa ushahidi wake kupitia kanda ya video. Kwa sasa Saif anazuiliwa na kundi moja la waasi la zamani katika mji wa Zintan ambapo wamekataa kumuachilia huru.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mrembo akuhumiwa jela kwa video tata mtandaoni

$
0
0

Mnenguaji wa kike nchini Misri, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuonekana kwenye video yenye utata mtandaoni.   Hukumu hiyo imetolewa na mahakama moja nchini humo kwa kosa la kuchochea ngono baada ya kuonekana katika video yenye utata katika mtandao.   Mrembo huyo aliyetambulika kwa jina la Reda al – Fouly alitiwa mbaroni, mara baada ya video hiyo ya miondoko ya Pop kuoneshwa hadharani na baadaye kudhihakiwa kuwa imeenda kinyume na tamaduni za kiarabu.   Muimbaji huyo wa kike alitakiwa kufafanua mavazi -aliyoyava kwenye wimbo unaoitwa Sib Eddi au let it go of my hand.   Hata hivyo inadaiwa kuwa mkurugenzi wa video hiyo, Wael Seddiki , aliondoka nchini Misri wakati wimbo huo ulipoanza kupondwa kwenye mitandao ya kijamii ili kukwepa lolote ambalo lingeweza kutokea..

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Kada mkongwe wa CCM Ambaye Alikuwa Waziri Katika Serikali ya Mwl. Nyerere Atimkia CHADEMA

$
0
0

Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi na ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Nazar Nyoni (84), amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Nyoni ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Elimu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, alisema ameamua kujiunga na Chadema baada ya kuvutiwa na maneno ya wabunge waliomaliza muda wao, Tundu Lissu na Halima Mdee. Alikuwa akizungumza mbele ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Morogoro Mjini, wanachama na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha wagombea ubunge na udiwani wa Jimbo la Morogoro Mjini. Nyoni alisema licha ya kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na kiongozi serikalini tangu mwaka 1975 hadi 1994 huku akiwa na kadi mbili ya Tanu na CCM, amemua kujiunga na Chadema pia baada ya kufuatilia mambo mengi ya msingi ikiwamo Bunge la Katiba na Bunge na kutambua kuwa chama kimoja chenye umoja na mbinu moja ni Umoja wa Katiba wa Wananchi (Ukawa). “CCM kwa sasa imechoka na kubaki kula fedha za nchi na kwa msingi huo, nikiwa mzee, nimeamua kuhamia Ukawa ili niseme kabla sijaaga dunia kuwa hakuna chama kinachoweza kuongoza Tanzana kwa sasa zaidi ya Chadema ama Ukawa,” alisema Nyoni. Awali, mtia wa kugombea ubunge Jimbo la Morogoro Mjini kupitia Chadema, Marcos Mgweno, aliwaasa wana-Morogoro kuukataa unyonge walionao kwa sasa kwa kuichagua Chadema kwa ajili ya maendeleo yao. Mgweno alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri duniani lakini utajiri huo hauwanifaishi wananchi husika bali wachache kwa manufaa yao binafsi. Naye Katibu wa Chadema Wilaya Morogoro Mjini, Esther Tawele, aliwataka wakazi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla, kutambua kuwa hatma ya maisha yao ipo mikononi mwao hivyo ni nafasi yao kutumia Ukawa katika kuwaletea mabadilko.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Hatupo tayari kuungana na chama kingine – TLP

$
0
0

Chama cha TLP kimesema hakipo tayari kuungana na chama kingine chochote kile kwa makubaliano ya kumsimamisha mgombea mmoja badala yake kitasimamisha mgombea wake makini ambaye ataingia katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya urais. Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha TLP taifa Dominata Rwechungura wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kishogo wilayani Bukoba ambapo amewataka watanzania kuendelea kuwa na imani na chama hicho huku akiwasisitiza wananchi kutowasikiliza wanasiasa wanaopanda kwenye majukwaa na kuwarubuni. Rwechungura ametoa tahadhari kwa watanzania ili wasikubali kununuliwa kwa gharama nafuu na wanasiasa wanaopitisha pesa kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa hali ambayo inaweza kusababisha kupata viongozi wabovu wasio na sifa ya kuliongoza taifa. Katika hatua nyingine naibu katibu mkuu wa TLP Dominata Rwechungura amelaani vikali juu ya wanasiasa wanao jilimbikizia pesa za walipakodi ambazo zilitakiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi huku makamu mwenyekiti wa TLP taifa Bw. Joas Kayura akiwataka watanzania kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kutochagua viongozi wabovu badala yake wawe makini na kuchangua viongozi wazalendo wenye sifa za kuliongoza taifa kwa umakini

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mbunge Mwingine wa CHADEMA Arudisha Kadi na kujiunga na CCM

$
0
0

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere ameng’atuka rasmi jana katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia alisema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko. Alisema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.   “Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia” amesema Leticia. Leticia alisema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge. Alisema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi. 

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

CCM Kumjibu LOWASSA Leo

$
0
0

Baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kutangaza kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na kuhamia Chadema jana katika ukumbi wa Bahari Beachi jijini Dar es salaam, chama cha Mapinduzi kimetoa taarifa ya kuzungumza na Vyombo vya Habari  leo.   Taarifa hiyo ya chama cha Mapinduzi haijafafanua kuwa ajenda itakuwa nini katika kikao hicho lakini kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kujibu shutuma zilizotolewa na Lowassa kuhusiana na madai ya kuwepo uonevu wakati akiomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CCM.   Mtandao huu utakujulisha kitakachojiri katika mkutano huo.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

LOWASSA CHADEMA: Fitina zimempeleka Lowassa upinzani

$
0
0

Hatimaye waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amekitosa chama chake cha CCM na kutua Chadema. Huko ndiko anatarajia kuendelea na safari yake ya matumaini aliyoianza na sasa anatarajiwa kupambana na ikiwezekana kukidhoofisha chama kilichomlea katika harakati za kuingia Ikulu. Serikali ya CCM ilimpa fursa nyingi za uongozi kuanzia ukurugenzi katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) na uwaziri. Amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sheria na Bunge 1990–1993), Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi (1993–1995), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Umaskini 1997–2000), Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo (2000–2005) na Waziri Mkuu (2005–2008). Alipata kila aina ya msaada aliouhitaji, akawa na nguvu za kiutendaji, kudhoofisha upinzani katika jimbo lake na hata kuthubutu kufanya maamuzi magumu katika nafasi mbalimbali alizoshika. Lakini baada ya kufanyiwa fitina wakati wa mchakato wa kuteua mgombea urais kupitia CCM, mbunge huyo wa Monduli tangu 1990 ameamua kuungana na wapinzani kuitia adabu CCM. Lowassa atakuwa kada wa tatu mwenye nguvu kuitikisa CCM na kuidhoofisha katika baadhi ya maeneo. Makada wengine waliowahi kuitesa CCM, kwa upande wa Bara ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustine Mrema; na kwa Zanzibar aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi, Seif Sharrif Hamad. Je, Lowassa ataujenga upinzani? Je, anaingia Chadema peke yake au pamoja na mafuriko ya watu waliokuwa wanakanyagana kumdhamini alipokuwa anagombea urais kupitia CCM? ni maswali ya msingi kujiuliza. Makada kadhaa wamewahi kujiondoa CCM na kujiunga na upinzani lakini yeye anakuwa kada wa kwanza aliyewahi kuwa waziri mkuu kukihama chama tawala Mrema ndani ya NCCR Upinzani dhidi ya chama tawala nchini una historia ndefu. Kada wa kwanza kupinga sera za chama tawala ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Oscar Kombona enzi za Tanu na kwa kuwa mfumo wa vyama vingi uliharamishwa mwaka 1965, alikosa sehemu ya kupumulia hivyo alikimbilia uhamishoni, Uingereza. Miaka ya 1980 waliibuka wanaccm kadhaa waliotaka mabadiliko, akiwamo mwasisi wa Chama cha Wananchi (CUF), James Mapalala. Harakati zake zilihesabika kuwa uhaini hivyo watu waliogopa kujiunga naye hasa walipomwona akikamatwa na kuwekwa kizuizini mara kwa mara. Miaka ya mwanzoni mwa 1990 akajitokeza Mrema. Kwanza, alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu, alikuwa kizuizi cha mageuzi. Pamoja na vigingi hivyo, mwaka 1991 wanaharakati walianzisha vyama vya kiharakati. Mapalala alianzisha Chama cha Wananchi na wengine kama Mabere Marando wakianzisha National Committee for Constitutional Reforms (NCCR) ambayo baadaye iligeuzwa kuwa chama cha NCCR-Mageuzi. Waanzilishi waliotoka CCM walikejeliwa kwa kuitwa majina kama vibaraka waliotumwa na mataifa makubwa kuisambaratisha nchi; malaya tu wa kisiasa. Pia walifananishwa na mchwa ambao watakufa kwa jua kali kwenye mwamba.  Haikutosha. Siku Mrema alipotembelea kwa helikopta wilaya ya Namanyere, Rukwa na kukuta imesimikwa bendera ya NCCR, alirejea Dar es Salaam na mikakati ya kuiangamiza kabla haijawa tishio. Baadhi ya wajumbe wakashawishiwa kujiondoa waanzishe vyama vyao ili NCCR idhoofike. Ikawa hivyo, mmoja aliasisi UMD huku waliobaki waliibadilisha NCCR na kuunda chama kwa jina la NCCR-Mageuzi, kikipewa maana ya National Convention for Construction and Reform yaani Chama cha Mageuzi na Ujenzi wa Taifa. Baada ya upinzani kuruhusiwa rasmi Julai 1992 vikasajiliwa vyama vingine kama DP, FORD, NLD, NRA, PONA, Tadea, UPDP, CUF, Chadema, TLP, na UDP na vingine vinaendelea kusajiliwa. Pili, mambo yalipokuwa magumu serikalini Mrema aliitosa CCM na kuipaisha NCCR alipojiunga nayo mwaka 1995 na akateuliwa kuwa mgombea urais. Mrema alipeleka mawimbi mazito CCM lakini kwa vile hakuwa na mtaji wa wanaccm aliohama nao, kura hazikutosha kumwezesha kuongoza nchi. Hata hivyo, aliingiza wapinzani kadhaa bungeni miongoni mwao ni waliojiondoa CCM kama Steven Wassira (Bunda), Makidara Mosi (Moshi Mjini), Dk Masumbuko Lamwai (Ubungo), Wengine ni Thomas Ngawaiya (Moshi Vijijini), Festus Limbu (Magu), MwinyiHamisi Mushi (Siha), James Mbatia (Vunjo), Paulo Ndobho (Musoma Vijijini), Mfalamagoha Kibasa (Iringa Mjini), Marando (Rorya) na wengineo. Mapalala na Hamad Baada ya Mapalala kukutana na viongozi wa chama cha Kamahuru ya Zanzibar kuunda Chama cha Wananchi (CUF), hakudumu, aliondolewa baada ya kutokea kutoelewana na wenzake. Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad ndiye alibaki kuwa nguzo imara ya chama hicho na kutikisa kuta za CCM visiwani Zanzibar. Kama ilivyokuwa kwa Mapalala, Maalim Seif amepitia masahibu mengi ya kutisha lakini yu imara hadi leo. Alipokuwa CCM alikuwa madhubuti, kiongozi mwenye mvuto na aliyeamini katika misingi. Hata hivyo, uamuzi wake wa kuwania urais wa Zanzibar kupambana na Mzee Idrid Abdul Wakil uliwachefua CCM. Wakamfitinisha. Januari 1988 alitemwa kwenye Baraza la Mapinduzi na akavuliwa cheo cha Waziri Kiongozi. Mei 1988 akafukuzwa uanachama wa CCM pamoja na wenzake sita kutoka Baraza la Wawakilishi. Mei 1989 alitiwa mbaroni na akafunguliwa kesi kwa madai ya kukutwa na nyaraka za siri za Serikali. Tangu mwaka 1989 hadi 1991 alikuwa mahabusu ya Polisi Zanzibar. Pamoja na mateso hayo, Maalim Seif amejenga upinzani wa nguvu Zanzibar na kuitokomeza CCM kisiwani Pemba akishirikiana na makamanda kadhaa baadhi wakiwa ni waliowahi kukabiliwa na kesi ya uhaini kama  Zulekha Ahmed Mohamed, aliyewahi kuwa naibu waziri wa Fedha Tanzania, Hamad Rashid Mohamed, Machano Khamis Ali, Hassan Mbarouk Hassan, Mohamed Ali Maalim, Shariff Haji Dadi, Ramadhan Shamna Abdi, Soud Yusuf Mgeni, Said Zam Ali, Pembe Ame Manja, Abbas Zam Ali, Nassor Seif Amour, Abdallah Said Abeid na Zeina Juma Mohamed. Baadhi ya makada wa zamani wa CCM wanadai kuwa Maalim Seif hajawahi kushindwa katika chaguzi za Zanzibar, japokuwa hajaachiwa ikulu. Nguvu yake ilisababisha kubadilishwa katiba ili chama chake kishirikishwe katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Kwa upande wa Bara, CUF ilipata wafuasi wengi akiwamo Mwenyekiti, Prof Ibrahim Lipumba aliyerithi mikoba ya Musobi Mageni. Mwaka 2000 na 2005 amewahi kushika nafasi ya pili katika mbio za urais. Safari ya Lowassa Kwa wiki tatu sasa upepo wa siasa umekuwa ukivuma kwa Lowassa aliyetawala siasa za hapa nchini tangu mwaka 2008 alipojiuzulu nafasi ya waziri mkuu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya kampuni isiyo na uwezo wala mtaji ya Richmond kupewa zabuni ya kufua umeme wa dharura nchini. Kamati Maalumu ya Bunge chini ya Mwenyekiti, Dk Harrison Mwakyembe ilifanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha ripoti bungeni kwamba kulikuwa na mkono wa Lowassa katika utolewaji wa zabuni hiyo. Serikali inasema aliwajibika kisiasa. Lowassa hakuwa na neno alipokatwa kuwania urais mwaka 1995 lakini mazingira yaliyojitokeza ya kukatisha safari yake ya ikulu mwaka huu yamezua nongwa na kuteka siasa za nchi kwa wiki tatu sasa. Waliomkata wamekuwa wakihaha, bila mafanikio, kumsihi asihame chama. Amepuuza na ameamua kuondoka, tayari amepokewa na Ukawa ambao wanatarajia kumteua kugombea urais kupambana na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli. Safari yake ya matumaini ni kuishi ikulu. Matarajio ya Ukawa ni kupanga ikulu. Matarajio ya Watanzania ni kupata mabadiliko nje ya CCM. Ikiwa Lowassa atamega nusu ya wanachama na mashabiki wa CCM, chama hicho tawala kitaanza kuonja joto ya jiwe na kuwa chama pinzani. Dk Slaa na Dk Kabouru Watu wengine waliowahi kuhama CCM ni mwasisi wa Chadema aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Edwin Mtei na wanasiasa wengine kama Bob Makani. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ambaye mwaka 1995 alishinda kura za maoni ndani ya CCM katika jimbo la Karatu, lakini wenye chama walimtosa wakamteua Patrick Qorro (marehemu). Wananchi walimwambia Dk Slaa aende chama chochote watamfuta na alipojiunga na Chadema mwaka huo, akashinda na hadi leo CCM ni chama cha upinzani Karatu. Wanasiasa wengine mashuhuri waliowahi kumeguka CCM ni aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Chadema Dk Amani Wallid Kabouru ambaye leo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Hotuba ya Lowassa kujiunga Chadema

$
0
0

Ndugu waandishi wa habari na ndugu Watanzania wenzangu. Yamepita majuma mawili tangu mchakato wa kuchagua mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ukamilike. Nimetumia muda huu kutafakari kwa kina yaliyotokea Dodoma na hatima yangu katika siasa nchini. Ninajua marafiki wengi na wananchi wenzangu wanaoniunga mkono wamekuwa wakisubiri kwa hamu nitoe kauli. Nilipokuwa natangaza nia ya kugombea urais kule Arusha, nilieleza nia yangu ya kuanza mchakamchaka wa maendeleo ya nchi yetu na kuondokana na umaskini. Pamoja na yaliyotokea Dodoma, azma hii bado iko palepale. Lakini nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyetupa sisi pumzi ya kuendelea kuwa wazima wa afya njema hadi hivi sasa. Nawashukuru pia mke wangu Regina, wanangu, wanafamilia na marafiki wote kwa mapenzi, msaada na uvumilivu wao wakati wa kipindi hiki kigumu tunachopitia. Nawashukuru sana pia maelfu ya wanachama wa CCM walionidhamini na mamilioni zaidi walioniunga mkono. Katika safari zangu za mikoani wakati wa kuomba udhamini, nilitiwa hamasa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kuniunga mkono.Aidha, ninawashukuru sana wana kamati wangu, makundi mbalimbali na mamilioni ya vijana wakiwamo; “For You Movement”, “Friends of Lowassa” “Team Lowassa”, Umoja wa Bodaboda na wengine wengi ambao walijitolea kwa hali na mali katika Safari yetu ya Matumaini. Nitakuwa sijahitimisha orodha ya shukrani iwapo nitaacha kuwashukuru viongozi wa dini zote nchini ambao waliungana na waumini wao wengi katika maombi na kwa kuniunga mkono. Najua sote tumevunjika moyo kwa yaliyotokea Dodoma na mazingira yaliyopelekea matokeo yale. Kama ilivyokwishaelezwa, mchakato wa kuteua wagombea uligubikwa na mizengwe, ukiukwaji wa maadili, uvunjaji wa Katiba na taratibu za uchaguzi za CCM. Zaidi ya hayo uchaguzi ulisimamiwa kwa upendeleo dhahiri na chuki iliyokithiri dhidi yangu. Kikatiba, Kamati ya Maadili si chombo rasmi na haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza majina miongoni mwa wale wanaoomba kugombea Urais kupitia CCM. Kilichotokea Dodoma ni kupora madaraka ya Kamati Kuu na kukiuka katiba ya CCM. Aidha, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu viliitishwa na kuburuzwa ili vitekeleze azma ya watu binafsi pasipo kujali demokrasia, katiba, kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM. Niliwekewa mizengwe na kuzushiwa majungu na uongo mwingi, kuhakikisha kuwa jina langu halifikishwi mbele ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu kujadiliwa licha ya ukweli usiopingika kuwa nilikuwa mgombea anayeungwa mkono na wananchi na wanachama wengi wa CCM kuliko wenzangu wote. Kibaya zaidi ni kile kitendo cha kuwanyima wagombea wote 38 haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu. Ni dhahiri kwamba njama dhidi yangu ndani ya CCM si jambo jipya.Kumekuwa na mkakati wa siku nyingi wa kulichafua jina langu kwa uzushi na uongo usio na kifani. Aidha, mmeshuhudia jinsi vijana kadhaa walivyotumika kunikashifu na kunitukana na bila aibu na uongozi wa CCM na Serikali kuwazawadia madaraka makubwa. Kwa namna ya kipekee napenda kuwapongeza na kuwashukuru wazee wetu akiwamo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na baadhi ya  wajumbe wa Kamati Kuu ikiwa ni pamoja na waheshimiwa Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Alhaj Adam Kimbisa kwa uadilifu na ushujaa wao mkubwa wa kuisimamia katiba ya CCM na misingi ya haki na kukataa maamuzi batili ya Kamati ya Maadili na Kamati Kuu kuhusu uteuzi wa wagombea. Cha msingi kuzingatia ni kuwa ili kuhitimisha njama za kunipora mimi na wagombea wengine haki zetu za msingi za kusikilizwa, viongozi wachache walikuwa tayari kupanda mbegu ya chuki na mfarakano ambao ni mfano mbaya kwa CCM na hata Taifa letu. Watanzania walitarajia chama kinachoongoza nchi kiwe ni mfano wa utawala wa sheria na kinara katika kutetea misingi ya haki na demokrasia na siyo kuihujumu. Yaliyotokea Dodoma yameitia dosari nchi yetu. Kwa kifupi, ninaamini sikutendewa haki katika mchakato mzima wa kupendekeza majina na kuteua mgombea wa urais kupitia CCM. Nilinyimwa haki yangu ya msingi ya kusikilizwa na kuchaguliwa. Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM au kuwa CCM ni chama kitakachowaletea ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu. Ni dhahiri kwamba CCM imepotoka na kupoteza mwelekeo na sifa ya kuendelea kuiongoza Tanzania yetu. Mimi kama Mtanzania aliye na uchungu na nchi yake nasema imetosha na SASA BASI! Kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyosema, CCM siyo baba yangu wala mama yangu na kwamba kama Watanzania hawapati mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Sasa tuyatafute mabadiliko nje ya CCM. Hivyo basi, baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu. Navishukuru vyama vyote vya siasa chini ya Ukawa, yaani Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa mwaliko wao na imani yao na kuthamini mchango ninaoweza kutoa kufanikisha azma ya kuleta mabadiliko na maendeleo ya kweli ya Taifa letu. Waheshimiwa Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, Mheshimiwa James Mbatia na Emmanuel Makaidi asanteni sana. Ndugu zangu, sikuufanya uamuzi huu kwa pupa, lakini unafika wakati wa kuchukua maamuzi hata kama ni magumu  kwa kuamini fika kuwa ni kwa masilahi ya Taifa letu. Nimejiridhisha kuwa ndani ya Ukawa Taifa letu linayo fursa ya pekee na ya kihistoria kushinda Uchaguzi Mkuu ujao na ya kuleta mabadiliko ya msingi katika nchi yetu. Kwa uamuzi na ushiriki wangu huu, ninaamini kwa dhati kuwa tutaondoa uhodhi wa madaraka wa chama kimoja na kujenga demokrasia yenye ushindani wa kweli kisiasa. Namalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania wenye nia njema na nchi yetu na wanaotaka kujenga demokrasia na kuleta mageuzi na maendeleo ya kweli, kujiunga nasi katika safari hii mpya ya kuinusuru nchi yetu. Safari ya Matumaini inaendelea kupitia Ukawa lakini haitafanikiwa iwapo sote hatutajiandisha kupiga kura. Natoa wito kwa wakazi wa Dar es salaam, kutumia fursa iliyopo kujiandikisha kwa wingi. Aidha, nawakumbusha Watanzania kote nchini waliojiandikisha kutunza shahada zao na kukumbushana kupiga kura ili ifikapo Oktoba mwaka huu tupate ushindi wa kishindo. Ndugu zangu Watanzania, tuungane pamoja kuuondoa umaskini na kuleta mabadiliko ya kweli. NA RUDIA CCM SIYO MAMA YANGU

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mwigulu ahojiwa na Takukuru kwa rushwa

$
0
0

Singida/Tanga. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Singida, inamhoji Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kwa tuhuma za kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Sheria ya Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007. Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Joshua Msuya alisema kwenye taarifa yake kwa umma na vyombo vya habari jana kuwa Mwigulu alianza kuhojiwa na Takukuru Wilaya ya Iramba kuanzia juzi na hadi jana alikuwa bado anaendelea kuhojiwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Hata hivyo, Mwigulu alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alisema Takukuru ilikuwa imeandaa kikao cha usuluhishi miongoni mwa wagombea wa vyama vyote baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka miongoni mwao. “Kuna baadhi walilalamika hadi kususia kampeni lakini tumesuluhishwa na tunaendelea na kampeni,” alisema. Hivi karibuni wapinzani wa Mwigulu, David Jairo, Amon Gyuda na Juma Kilimba, walipeleka malalamiko Takukuru kuwa Mwigulu amekuwa akitoa ahadi za kuwapa wananchi wa jimbo lake pikipiki, baiskeli na kukarabati barabara kwa fedha zake katika kipindi cha kampeni, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za uchaguzi. Msuya aliwatahadharisha wagombea wa udiwani na ubunge mkoani hapa kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye kampeni za kura za maoni na Uchaguzi mkuu. Alisema watakaobainika kukiuka sheria hiyo kwa kutoa rushwa ya fedha taslimu, madawati, vifaa vya michezo au rushwa ya aina nyingine yoyote, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Takukuru Tanga yaonya Uongozi wa Takukuru Mkoa wa Tanga, umedhamiria kuwabana wagombea ubunge na udiwani kutokana na malalamiko kwamba baadhi wamekuwa wakitoa rushwa. Tayari taasisi hiyo imeanza kuwahoji baadhi ya wagombea wanaotuhumiwa huku ikifuatilia kwa siri michakato ya uchaguzi katika vyama vyote vya siasa pamoja na kutoa elimu ya Sheria namba 6 ya Uchaguzi ya mwaka 2010. Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tanga, Aidano Ndomba alisema jana kuwa wagombea watambue kwamba taasisi hiyo ipo kazini na itawabana wote watakaobainika kutoa au kupokea rushwa. “Tumeanza kuchukua hatua ya kuwahoji na kukusanya ushahidi kwa baadhi ya wagombea ambao wamelalamikiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa,” alisema Ndomba na kusisitiza kuwa maofisa wa Takukuru wanafuatilia kwa siri michakato yote.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Wema sikendo za ngono basi!

$
0
0

Kufuatia kupigwa mwereka kwenye Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekiri kwamba kilichomponza katika kinyang’anyiro hicho ni skendo za ngono hivyo kwa sasa atakuwa makini ili asichafuke. MAPOKEZI Akizungumza na mtandao huu baada ya kupokelewa kishujaa na kuacha historia jijini Dar aliporejea kutoka Singida wikiendi iliyopita, Wema alisema mashabiki wake hawatamsikia tena na skendo hizo huku akiahidi kuibuka na bonge la ‘surprise’. UMAKINI “Shukurani zangu zipo palepale kwa mashabiki wote wanaonisapoti. “Ninachowaahidi kwa sasa ni kuwa makini na skendo lakini pia kuna kitu cha kushtua nitafanya hivi karibuni ambacho kitaibua surprise (mshtuko) nzito kwa mashabiki wangu,” alisema Wema. Mashabiki wakiwa na Wema wakati wa mapokezi. TEAM WEMA Katika mapokezi hayo ambayo gazeti hili lilikuwa mstari wa mbele, makundi ya mashabiki wake na yale ya Team Wema yalipeana taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kipenzi chao, Wema angefika Dar, Jumapili iliyopita ambapo taarifa zilisema kuwa walikutana kimyakimya na kuandaa mapokezi ya Madam. Mishale ya saa 7:00 mchana ndipo Team Wema na mashabiki wake wengine walianza kumiminika maeneo ya Kimara-Baruti jijini Dar wakiwa na mabasi ya kukodisha, pikipiki na magari binafsi ambapo shamrashamra za kila aina zilifanyika. KIBAO-KATA Pia kulikuwa na ngoma ya Kibao-Kata, michezo ya pikipiki huku nyimbo za kumsifu Wema zikiimbwa. Kama hiyo haitoshi, amshaamsha hiyo ilikuwa ikifanywa kila sehemu ambapo mastaa walikuwa wakitokea maeneo hayo kwa ajili ya kumsapoti Wema. SHANGWE Umati uliojitokeza walianza kulipuka kwa shangwe baada ya kumuona Meneja wa Wema, Martin Kadinda aliyeingia katika eneo hilo akifuatiwa na Petit Man ambaye alifuatana na wasanii wa Bongo Fleva, Mirror na Suma Mnazareti. MJAMZITO Mashabiki hao wa kila kada huku watoto wakifurika kumuona Wema walionekana kuwa na mapenzi ya hali ya juu huku mama mmoja mwenye ujauzito mkubwa akionekana akijichanganya kila kona bila kujali hali yake. WEMA ENEO LA TUKIO Wema aliingia katika maeneo hayo (Kimara-Baruti) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser ambapo alishuka na kuingia ndani ya BMW lililoletwa kumpokea ambapo alitokea kwenye paa na kuanza kusalimia mashabiki wake waliolipuka kwa furaha na wengine wakiangua kilio cha furaha. MABUSU Kuna wengine walishindwa kujizuia wakajikuta wakimfuata Wema wakimbusu na kumshika nywele zake kama vile siyo binadamu. CHENI NA PETE Wema alilazimika kugawa cheni na pete zake za dhahabu kwa mashabiki wake ili kuwatuliza huku akiwashukuru kwa kumpokea na kuwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwake Kijitonyama ambapo msafara wake ulisababisha foleni ya zaidi ya robo saa njia nzima ambapo alikuwa akisindikizwa na pikipiki. “Yaani Madam amepokelewa na watu kama rais vile, duh! Sijawahi kuona, amekosa ubunge lakini shamrashamra yake kama vile ameshinda!” Alisema mmoja wa mashabiki wa Wema aliyevalia fulana zenye nembo iliyoandikwa ‘Wema’. KINACHOONEKANA Habari zilieleza kwamba, kinachoonekana Wema anajipanga upya ili kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya baadaye hivyo atajitahidi kuwa mbali na skendo hasa za wanaume. TUJIKUMBUSHE Huko nyuma Wema aliwahi kuripotiwa kubadili wanaume mbalimbali wakiwemo; Jumbe Yusuf Jumbe, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na CK.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Mapacha wa Shija wawachanganya mabwana

$
0
0

WACHINA! Kutokana na kufanana sura na maumbo waigizaji wa filamu Bongo ambao ni mapacha, Christina Mroni na Regina Mroni ‘Mapacha wa Shija’ wamewaweka katika wakati mgumu marafiki zao wa kiume baada ya kuwachanganya wasijue nani ni nani. Mmoja wa mapacha hao, Christina alisema wanaume wao wamekuwa wakichanganyikiwa kutokana na kufanana kwao kwani hivi karibuni alikwenda ofisini kwa pacha mwenzake, lakini shemeji yake alipofika hapo alitaka kumkumbatia kimahaba akiamini ni mpenzi wake ambapo alilazimika kumkwepa. “Mwenzangu alikataa na kukimbia akimwambia kwamba siyo yeye ndipo nikamwambia mimi ndiye mpenzi wake, akabaki ameduwaa, Mungu ni wa ajabu sana kwani hata watoto wetu ni wa kiume na wamepishana miezi miwili tu, nao wanafanana, tuna malengo ya siku zijazo tuwe  mapacha maarufu duniani,”alisema pacha huyo ambaye pamoja na mwenzake wameandaa filamu yao mpya inayoitwa Dada.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Muandishi Wa habari Amfukuzisha Kazi Kocha Wa Mexico

$
0
0

Shirikisho la soka nchini Mexico (FMF), limemfuta kazi kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Miguel Herrera, baada ya kujiridhisha alionyesha utovu wa nidhamu wakati wa kufurahia ubingwa wa ukanda wa Amerika ya kati, kaskazini na visiwa vya Caribbean (CONCAFAC Gold Cup) mwishoni mwa juma lililopita.   Raisi wa shirikisho la soka nchini Mexico akiongeza na waandidhi wa habari. Raisi wa shirikisho la soka nchini humo Decio de Maria, alithibitisha kumfuta kazi kocha huyo kwa kusema Herrera amebainika alimsukuma muandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Mexico (TV Azteca), Christian Martinoli ambaye kila wakati alikiponda kikosi cha mabingwa hao wa CONCACAF. Decio de Maria, amesema wamechukua maamuzi hayo baada ya kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumuhoji Herrera na Christian Martinoli ambapo kila mmoja alieleza uhalisia wa tukio lilivyokua. mwandishi anayedai kusukumwa na kocha wa mexico Tukio la kusukumwa kwa Christian Martinoli lilitokea kwenye uwanja wa ndege Philadelphia wakati wa safari ya kikosi cha Mexico kilipokua kikirejea nyumbani. Hata hivyo rais wa shirikisho la soka nchini Mexico, De Maria amesema kocha Herrera baada ya kufanya hivyo aliomba radhi kupitia katika kituo kimoja cha radio cha nchini Mexico, lakini haikutosha kuwashawishi kukubali msamaha huo alisukumwa na Herrera, alianza kukikandia kikosi cha timu ya taifa ya Mexico, baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye michuano ya Ukanda wa Amerika ya kusini (Copa Amerika) iliyofanyika nchini Chile, hususan walipotolewa katika hatua ya makundi. Kufuatia maamuzi ya kutimuliwa kwa Miguel Herrera, kunaufanya uongozi wa shirikisho la soka nchini Mexico kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wake, na tayari rais De Maria amesisitiza kuhitimisha zoezi hilo itakapofika mwezi Septemba. Mexico walitawazwa kuwa mabingwa wa CONCACAF Gold Cup mwaka 2015 baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Jamaica mabao matatu kwa sifuri katika mchezo wa hatua ya fainali uliounguruma mjini Philadelphia nchini Marekani mwishoni mwa juma lililopita.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat

Viewing all 2247 articles
Browse latest View live