Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Maamuzi mapya ya Kocha wa Taifa Stars dhidi ya Mbwana Samatta siku mbili baada ya ushindi wa tuzo (+Audio)

$
0
0

Siku mbili baada ya mshambuliaji kimataifa wa  Tanzania  anayekipiga katika klabu ya  TP Mazembe  ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  Mbwana Samatta  atangazwe na shirikisho la soka barani  Afrika CAF  kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa  Afrika wa mwaka 2015 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika. Charles Boniface Mkwasa January 10 uwanja wa  Amaan  visiwani  Zanzibar  kocha wa timu ya taifa ya  Tanzania Taifa Stars   Charles Boniface   Mkwasa  ametangaza kumteua  Mbwana Samatta  kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya  Tanzania Taifa Stars . Uamuzi huo wa  Mkwasa umekuja siku mbili baada ya  Samatta  kutwaa tuzo. Kwa sasa  Nadir Haroub   atakuwa nahodha wa timu ya  CHAN   na  John Bocco  atakuwa nahodha msaidizi wa  Samatta . “Ni mabadiliko ya kawaida hasa baada ya Mbwana kutwaa tuzo na heshima kubwa kwa Afrika, sisi tumeona tumuongezee majukumu mengine ili aweze kutuongozea timu yetu ya taifa Taifa Stars, ameweza kuiongoza TP Mazembe kuwa Bingwa wa Afrika, hivyo tumeona tumpe fursa hii ili awaongoze wenzake katika mechi za AFCON zilizobaki” > > > Mkwasa Unaweza msikiliza hapa  Charles Mkwasa

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles