Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Yanga yaondolewa na URA ya Uganda nusu fainali, Alikiba jukwaani akishuhudia (+Pichaz)

$
0
0

Saa chache baada ya mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2016 kumalizika, kwa klabu ya  Mtibwa Sugar  ya Manungu Turiani kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kuweka rekodi ya kuingia fainali yake ya tano ya michuano hiyo. Usiku wa January 10 klabu ya  Dar Es Salaam Young African  nayo ilishuka dimbani kucheza mchezo wa nusu fainali ya pili dhidi ya klabu ya  URA  ya  Uganda  katika dimba la Amaan , mchezo ambao ulikuwa unamtafuta bingwa mmoja kati ya timu hizo kwenda kucheza dhidi ya  Mtibwa Sugar  katika hatua ya fainali ya michuano hiyo. Yanga  ambayo ilikuwa inaongoza katika msimamo wa  Kundi A  ilianza kwa kupachika goli la uongozi dakika ya 13 kupitia kwa  Amissi Tambwe  ambaye aliutumia vyema mpira uliopigwa kichwa na  Simon Msuva  na kushindwa kutinga nyavuni, kipindi cha pili  URA waliendelea kuwa na nidhamu ya mchezo, licha ya kuwa walikuwa nyuma. Ali Kiba  akiwa jukwaani akishuhudia mchezo wa Yanga dhidi ya URA URA  walifanikiwa kupata goli la kusawazisha dakika 14 kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa  Peter , hadi dakika 90 zina malizika  Yanga  1-1  URA . Katika hatua ya mikwaju ya penati  Geofrey Mwashiuya  na  Malimi Busungu   walikuwa hawana bahati, kwani walikosa penati, lakini  URA  mchezaji aliyekosa penati alikuwa ni  Sekito Sam  pekee.  URA imeifuata  Mtibwa Sugar  fainali kwa kuibuka na ushindi wa penati 4-3.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles