Wakala wa mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi, Robin van Persie, amekanusha taarifa za mchezaji wake kuhusishwa na mipango ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Fenerbahce, ya nchini Uturuki. Kees Vos, wakala wa mshambuliaji huyo amesema taarifa zilizoanza kutolewa na baadhi ya mitansdao ya habari zinazoeleza juu ya uhamisho wa Van Parsie hazina ukweli wowote. Mwishoni mwa juma lililopita, The Guardian walilipoti kwamba Van Persie amekubaliana na viongozi wa klabu ya Fenerbahce, maslahi yake binafsi na kinachosubiriwa kwa sasa ni makubaliano baina ya upande huo wa uturuki dhidi ya Man Utd. Vos, amesema taarifa hizo zimemsikitisha sana, kutokana na aliyeziendika kutokujua ukweli wa mambo dhidi ya mchezaji wake. Van Parsie mwenye umri wa miaka 31, amekua akihusishwa na taarifa za kuondoka Old Trfford katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, na tayari imeshaanza kuzungumzwa huenda akauzwa kwa ada ya uhamisho wa paund million 5. Tayari mshambuliaji wa pembeni wa Man Utd, Luis Nani ameshakamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Fenerbahce, na jana jioni alipata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat