Quantcast
Channel: Paul Joseph – AutomobileHeat
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Sentensi 10 za mke wa Marehemu kuhusu ajali, picha za Marehemu na kifo cha Mchungaji Mtikila..

$
0
0

October 22 2015  ni wiki ya tatu zimepita tangu aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha Democratic Party  (DP) Mchungaji  Christopher Mtikila  afariki kwa ajali ya gari ndogo eneo la  Msolwa , Chalinze Mkoa wa Pwani. Rais JK  akimpa pole Mama  Georgia Mtikila  siku mwili wa Marehemu  Mtikila ulipoagwa Viwanja vya  Karimjee Dar . Mama  Georgia Mtikila  ni mke wa Marehemu  Mchungaji Mtikila … leo kwa mara ya kwanza amekutana na Waandishi wa Habari Dar es Salaam na kuzungumzia kuhusu kifo cha mumewe > > > > “ Kuna habari ilitoka kwamba familia imesema ajali ya Mchungaji Mtikila ni ya kawaida.. naipinga, aliyetoa taarifa hiyo hakuwa mwanafamilia na sio Mwanachama wa DP… Hakuna Mwanafamilia aliyekuwa tayari kutoa taarifa yoyote kwa niaba ya Chama wala Familia .” “ Naomba tusaidiwe ili haki ya Marehemu ionekane ikitendeka, haya maombi tunaomba yafike…. Tunaomba Rais aingilie kati kwa kuunda Tume huru isiyohusisha Polisi ili kuchunguza kifo cha Mchungaji Mtikila ” > > >   Mama  Georgia Mtikila . Marehemu Mchungaji  Christopher Mtikila . “ Tunaiomba TCRA itusaidie kumpata mtu aliyeweka picha ya Marehemu Mtikila alfajiri siku ya ajali, kwa sababu mpaka sasahivi simu ya Mchungaji hatujui iliko… ” > > >  Mama Georgia Mtikila .

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2247

Trending Articles